Taka zilizokusanywa Desemba 9 zizolewe kabla ya Desemba 20
Waziri George Simbachawene akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo mjini Dodoma
WAZIRI wa
nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George
Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurungenzi
wote wa halmashari nchini kuhakikisha wanazoa taka zote zilizokusanywa
wakati wa siku ya uhuru kabla ya tarehe 20 mwezi huu.
Kauli
hiyo aliitoa wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo
wakati wa kikao cha kumkaribisha katika ofisi ya TAMISEMI mjini Dodoma.
Alisema kuwa hataki kuona hadi ifikapo tarehe 20 ya mwezi huu kuwa uchafu unaendelea kulalamikiwa:
“Hadi
ifikapo tarehe hiyo sitaki kusikia uchafu bado haujaondolewa katika
maeneo ulipokusanywa toka Siku ya Uhuru, lakini pia unapoondolewa huo
kuna uchafu mwingine unakuja hivyo basi watendaji wanaohusika
wahakikishe kuwa wanaanda maeneo ya kuupeleka,”alisema Simbachawene.
Naibu
Waziri wa wizara hiyo Suleiman Jaffo, aliwataka watumishi wa TAMISEMI
kubadilika katika utendaji wao wa zamani ili waweze kuongeza ukusanyaji
wa mapato na kuweza kuboresha maisha ya wananchi.
Comments
Post a Comment