Maafisa 16 wa FIFA kizimbani kwa ufisadi
Mwanasheria Mkuu nchini Marekani Loretta Lynch
Waendesha
mashtaka nchini Marekani wametangaza mashtaka mapya dhidi ya maafisa
wapatao kumi na sita wa shirikisho la kandanda duniani FIFA kwa kuhusika
na tuhuma za rushwa baada ya uchunguzi ndani ya shirikisho hilo.
Walioshtakiwa
ni pamoja na maafisa wa ngazi ya juu wa Kamati ya uongozi wanaoongoza
hivi sasa na wale waliostaafu akiwemo Rais wa chama cha soka cha
Honduras Rafael Callejas.
Mwanasheria
Mkuu nchini Marekani Loretta Lynch amesema katika miongo miwili maafisa
hao waliokula njama ya kula rushwa ndani ya shirikisho hilo ya dolla za
kimarekani milioni mia mbili.
"Baraza
la wazee wa mahakama wa Brooklyn wamerudisha mashtaka 92 katika Mashtaka
makuuu dhidi ya washtakiwa wapya 16 wote ni maafisa wa sasa na wa
zamani wa shirikisho la soka duniani. Kila mmoja katika hao maafisa 16
wameshtakiwa kwa kula njama ya kujipatia fedha kwa udanganyifu, na
makosa mengine kwa kutumia nafasi zao kujinufaisha kifedha."
Aidha amefafanua kiwango cha rushwa walichopokea ni ufisadi wa kiwango cha juu.
"Sasa
acha nisema uvunjifu wa uaminifu hapa ni ufisadi wa hali ya juu na
kiwango cha rushwa wanachotuhumiwa hapa ni wa kupitiliza.
Na ujumbe
katika tangazo hili uwe wazi kwa kila mtuhumiwa aliyebaki ambapo
tumewahifadhi wakidhani wanaweza kukwepa uchunguzi huu unaoendelea,
hatuwakusubiri na wala hawatakwepa lengo letu."
Aidha Kwa
upande mwingine, shirikisho hilo la soka duniani limesema litaendelea
kushirikiana na mamlaka nchini Marekani ambapo limetangaza mlolongo wa
mageuzi ndani ya shirikisho hilo.BBC
Comments
Post a Comment