Obama: Hatutayumbishwa na shambulio
Obama amesema Marekani iko imara
Rais Barack Obama amesema Marekani haitayumbishwa na shambulio la Jumatano katika mji wa San Bernardino, California.
"Sisi
tuna nguvu. Tuko imara," amesema kwneye hotuba yake ya kila wiki kupitia
redio, akisema inawezekana kwamba watu wawili waliofyatua risasi na
kuua watu 14 katika mji huo walikuwa wameingizwa kwenye itikadi kali.
Syed
Rizwan Farook, 28, na mkewe Tashfeen Malik, 27, walitekeleza mauaji hayo
kabla ya kuuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi katika yao na polisi.
FBI wanachunguza kisa hicho kama kitendo cha ugaidi.
Kundi la
wapiganaji wanaojiita Islamic State Jumamosi lilisifu shambulio hilo na
kusema lilitekelezwa na “watu wawili wanaounga mkono Islamic State".
Taarifa
hiyo iliyopeperushwa kupitia redio ya IS ya al-Bayan haikutoa ishara
zozote kuhusu kuhusika kwa kundi hilo kwenye shambulio hilo katika
sherehe ya Krismasi kituo cha Inland Regional Center.
"Tunajua
kuwa Isil (IS) na makundi mengine ya kigaidi yanawahimiza watu – kote
duniani na hata nchini mwetu – kutenda vitendo vibaya vya mauaji, wakati
mwingine kivyao,” Bw Obama amesema.
"Sote,
serikali, idara za usalama, jamii, viongozi wa kidini, tunahitaji
kufanya kazi kwa pamoja kuzuia tusipotoshwe na itikadi hizi za chuki.”BBC
Comments
Post a Comment