AZAM FC YAIPIGA 'MKONO' MTIBWA SUGAR

TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi mnono wa mabao matano 'mkono' dhidi ya mawili yaliyofungwa na Mtibwa katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mabao ya Azam yamefungwa na Didier Kavumbagu aliyetupia mawili pamoja na Frank Domayo ambaye naye amefunga mawili huku bao la mwisho likiwekwa kimiani na Kipre Tchetche.
Mabao mawili ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Musa Nampaka na Ameir Ally.
Kwa matokeo ya leo, Azam wamerudi tena kileleni wakiwa na jumla ya pointi 25 sawa na Yanga lakini wakiwazidi Yanga kwa tofauti ya mabao.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA