NYOTA WA SOKA DUNIANI KLUIVERT NA RAYCO GARCIA WAKUTANA NA STAND UNITED, SHINYANGA
![]() |
| Wachezaji wa Stand United wakiwasili Uwanjani |
Mji wa Shinyanga jioni ya jana ulitekwa na kocha namba mbili wa timu ya taifa ya Uholanzi 2014 ambye pia alikuwa mchezaji gwiji na nyota wa Ajax Amsterdam, Barcelona ya Hispania na New Castle ya Uingereza, Patrick Kluivert bingwa wa mipira ya vichwa aliyekuwa ameambatana na na gwiji wa zamani wa Barcelona na Real Madrid Rayco Garcia ambaye ni Scout wa Real Madrid kwa kukutana na wachezaji wa Timu ya Stand United ya Shinyanga pamoja na mashabiki wa soka kutoka ndani na nje ya mkoa huo katika kiwanja cha CCM Kambarage.
Tukio zima limefanikiwa chini ya udhamini wa mbunge wa Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayesimamia Muungano na Mazingira.
Lengo ni kusaka vipaji vya soka kwa ajili ya kucheza ligi za Ulaya, kukuza michezo na kuitangaza Shinyanga nje ya mipaka ya nchi.

Patrick Kluivert akisalimiana na wapenzi wa soka mkoa wa Shinyanga wakati akipanda jukwaa kuu

Kulia ni Patrick Kluivert akifuatilia mazoezi yaliyokuwa yanafanya na wachezaji wa Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage kabla ya kuongea nao na kuwapa siri ya mafanikio katika soka ili waweze kucheza ligi za ulaya


Patrick Kluivert akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Stand United wakati wa zoezi maalum jioni ya leo lengo ni kuwanoa ili wawe tishio ndani na nje ya Tanzania

Wa kwanza kushoto ni afisa Habari wa Stand United Isaack Edward akifuatiwa na mkurugenzi wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde wakiwa na Patrick Kluivert wakifuatilia zoezi maalum la wachezaji wa Stand united

Mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akiwakaribisha magwiji wa soka ili wazungumze na mashabiki wa soka .


Patrick Kluivert akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema anataka kuisaidia timu ya Stand United ili iweze kupeleka wachezaji wake kucheza mechi za nje ya nchi.
Kwa picha zaidi, tembelea blogu ya Malunde: ANGALIA PICHA ZAIDI YA 10- TUKIO LILILOTIKISA MJI WA SHINYANGA LEO JIONI


Comments
Post a Comment