Posts

Showing posts from April, 2012

NAWATAKIA WEEKEND NJEMA

Nawatakia wapenzi wa blog hii weekend njema,kwa wale mnaoenda kanisani basi huu ndo muda muafaka wa kumkumbuka muumba wako kwani kwa week nzima ulikuwa busy kwa shughuli mbalimbali za kulijenga taifa hivyo basi muda huu wa mapumziko ya mwisho wa week utumie vizuri kwa kwenda kanisani au kutembelea ndugu na jamaa zako ambao umekuwa ukiwapigia simu tu na saa zingine kuwapigia kimya kabisa. WEEKEND NJEMA

KATUNI YA LEO......Hii kali!

Image

SAUT STUDENTS' PUBLIC RELATIONS ASSOCIATION (SSPRA) YAPATA VIONGOZI WAPYA

Image
Uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya wa SSPRA kwa mwaka 2012/2013 umefanyika katika ukumbi wa B1 mwanjonde lecture Theatre katika chuo kikuu cha Mt.Augustino. Uchaguzi huu umekuwa wa mafanikio makubwa sana kwa kuwa sheria zote za uchaguzi zimeweza kuzingatiwa na wapiga kura kuweza kulidhika na viongozi wote waliowachagua kwa kuwapatia idadi kubwa ya kura za NDIO kutoka kwa wapiga kura hao ambao idadi kamili ilikuwa ni 101.Yafuatayo ni majina ya viongozi wapya pamoja na vyeo vyao ndani ya SSPRA pamoja na idadi za kura walizozipata.  MWENYEKITI - CHRISTOPHER T. NGONYANI (BAPRM 2) amepata kura 100 za NDIO na kupata kura 1 ya HAPANA,,katika nafasi hii ya Mwenyekiti alikuwa mgombea pekee.  MAKAMU MWENYEKITI- MSEKWA B. CHEBY (BAPRM 2) amepata kura 99 za NDIO na 2 za HAPANA,katika nafasi hii alikuwa mgombea pekee.  KATIBU MKUU-MLAY P.MZEE (BAPRM 2)amepata kura 63 zidi ya Mwema F. Kihengu ambaye amepata kura 38,hivyo basi MLAY P.MZEE ndio KATIBU MKUU mpya wa nafasi hii ambayo

Kilimo Kwanza kimewafikia pia Wamasai

Image
Wamasai hawa ni Mfano kuigwa   si ufugaji tu hata kilimo wanaweza

BAADHI YA MARAIS WA (EAC) WAWASILI JIJINI ARUSHA

Image
Mhe. Mwai Kibaki, Rais wa Kenya akipokelewa na Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika mjini Arusha tarehe 28 Aprili, 2012. Mhe. Rais Kibaki akifurahia burudani ya ngoma mara baada ya kuwasili KIA. Mhe. Rais Kibaki akiwa na wenyeji wake Mhe. Membe (kulia) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta (kushoto) mara baada ya kuwasili KIA Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Uganda akisalimiana na Mhe. Samwel Sitta, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki mara baada ya kuwasili KIA kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 28 Aprili, 2012.   source www.fullshangweblog.com

SCHOLARSHIP PROGRAMME TO JAPAN.

Image
Greetings from the Embassy of Japan, The MEXT scholarship programme for study in Japan is available annually and information for the 2013 academic year has been posted on our webpage. Applicants for Undergraduate, Specialized Training and Research (Masters or PhD) studies are invited to visit our homepage, where they will find the required information and application forms. Kindly refer applicants to http://www.tz.emb-japan.go.jp/study.html   I attach a small poster which gives details of the programmes and request if you would be kind enough to distribute and display it at your institution (the deadline for submission is 15 June 2012). Should you or any students have queries, please feel free to contact us on  embassyofjapan_TZ@dr.mofa.go.jp   With thanks and best regards, Louise Tonkin Culture and Public Relations Embassy of Japan in the United Republic of Tanzania website:   http://www.tz.emb-japan.go.jp/index.html

KITIVO CHA ELIMU UDOM CHAIBUKA NA USHINDI WA VIKAPU 58 KWA 53 DHIDI YA DODOMA SPURS KATIKA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU MKOANI DODOMA

Image
Mchezaji wa Timu ya Mkoa alipoipatia timu goli katika ligi ya mpira wa kikapu iliyoanza leo katika viwanja vya kitivo cha sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha cha Chuo Kikuu Cha Dodoma Kashikashi ikiendelea hapo huku wengine wakitaka kushinda huku wengine wakitaka kuokoa goli lisiingie Mchezaji wa Timu ya Kikapu ya Dodoma Spurs (Timu ya Mkoa) akijaribu kumpita Mchezaji wa timu ya kikapu ya kitivo cha elimu cha chuo kikuu cha Dodoma katika mchezo wa ligi ya mpira wa kikapu iliyoanza leo na timu ya Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Cha Dodoma Chaibuka Mshindi Kwa Vikapu 58 kwa 53 Dhidi ya Timu ya Mkoa (DODOMA SPURS) Baadhi ya Wanafunzi na Wadau wengine wakifuatilia mchezo huo uliokuwa ukichezwa kati ya Timu ya Mpira ya Kikapu kutoka Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma Na Timu ya Dodoma Spurs (Timu ya Mkoa) ambapo timu ya kitivo cha elimu cha Chuo Kikuu Cha Dodoma iliibuka na ushindi wa Vikapu 58 kwa 53 dhidi ya Timu ya Mkoa Wa Dodoma (DODOMA SPURS) katika

HAPPY BIRTHDAY SONGORO MENEJA

Image
Leo ni birthday ya mdau wa blog hii anajulikana kwa jina maarufu "Meneja".....Kijana asiyekata tamaa mapema hata kama timu yake ya darasa imefungwa pia muamasishaji mkubwa pindi timu ya darasa BAPRM 2 inapokuwa kiwanjani inacheza. NAKUTAKIA BIRTHDAY NJEMA NA MUNGU AKUSIMAMIE KWA KILA JAMBO ULIFANYALO

MVUA KUBWA NDANI YA MWANZA YASIMAMISHA MECHI YA AND 1 NA MWANZA ALL STARS

Image
Kukosekana kwa viwanja vya ndani vimeligharimu jiji la Mwanza kukosa burudani ya Kimataifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa mchezo wa basketbal waliofurika katika dimba la CCM Kirumba hii leo mara baada ya mvua kubwa kunyesha hali iliyopelekea hali ya uwanja kuwa tete. Huku mashabiki wa basketbal wa jiji hilo la miamba wakiwa na kiu ya kushuhudia maufundi ya wachezaji wa Mwanza All stars na wale wakali kutoka nchini marekani And 1, ilikuwa ni majira ya kumi mvua kubwa ilinyesha kwa muda mrefu hata kusababisha eneo la uwanja kuwa si salama kwa wachezaji. Adam Mchomvu akishow love ndani ya blog   Nilimtafutaje Hot Sauce hapa nikatokelezea naye Maiko Maluwe ni Kaimu katibu mkuu shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania ambaye ameambatana na timu ya And 1 jijini Mwanza naye anaeleza sababu za katisho la mchezo huo.. . .   wachezaji wa And 1 wakipasha misuli kabla ya mvua kunyeesha Adam Mchovu na

"NIDANGANYE"- SHETTA Feat DIAMOND

Image
Mapenzi ni uongo??Ni swali gumu ambalo laweza kuwa jepesi pia!Usishangae na wala usibishe.Ndio ukweli.Kinyume cha hapo unaniongopea. Nidanganye . Kuna wakati lala lalal lalala za mapenzi hujaa uongo unaopendeza. Wenzetu wa huko mbele wanasema Sweet Nothings.Utupu. Ukweli unauma…nakupenda! Kuna wakati mapenzi hupumbaza.Unachoambiwa na mhusika ndicho unachokielewa na kukikubali. Nakupenda wewe zaidi ya mwingine.Unakubali hata kama kila mtu anakwambia sio kweli.Mpo wengi. Analosema ndio sheria.Ni wewe tu. Maudhui hayo ya mapenzi ndio yaliyomo katika wimbo mpya kutoka kwa Shetta akiwa amemshirikisha Diamond . Kama wimbo unavyoitwa Shetta na Diamond wanasema Nidanganye…ukiniambia ukweli roho itauma sana.Nitaumia. Diamond anasema kwenye chorus kwamba  hata akimkuta chumbani kakumbatiwa…mmmmh!! Hii ni production nyingine kutoka kwa KGT. < > (Shetta_ft_Diamond_-_Nidanganye.mp3)

DIAMOND AKAMUA NDANI YA GOLD CREST-MWANZA KATIKA HAFLA YA MAKATIBU MUHTASI

Image
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Diamond akizikonga nyonyo za mashabiki wake kwa moja ya nyimbo zake usiku huu,kwenye hafla ya jioni ya washiriki wa Kongamano la Makatibu Muhtasi nchini,iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.  Diamond akiendelea kutoa burudani kwa Mashabiki wake.  Diamond akiwa amenyanyliwa juu juu na Madansa wake,ikiwa  ni sehemu Gold Crest,Jijini Mwanza.  Diamond akigombewa na Mashabiki wake kama mpira wa kona.  Mwanamuziki Mkongwe wa Bendi ya The Kilimanjaro a.k.a Wana Njenje,Nyota Waziri akiimba nyimbo yake ya Gere wakati wa hafla ya jioni ya washiriki wa Kongamano la Makatibu Muhtasi nchini,iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku huu.  Mwanamuziki Mkongwe wa Bendi ya The Kilimanjaro a.k.a Wana Njenje,Nyota Waziri akiimba nyimbo yake ya Gere wakati wa hafla ya jioni ya washiriki wa Kongamano la Makatibu Muhtasi nchini,iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ho