SAUT STUDENTS' PUBLIC RELATIONS ASSOCIATION (SSPRA) YAPATA VIONGOZI WAPYA

Uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya wa SSPRA kwa mwaka 2012/2013 umefanyika katika ukumbi wa B1 mwanjonde lecture Theatre katika chuo kikuu cha Mt.Augustino. Uchaguzi huu umekuwa wa mafanikio makubwa sana kwa kuwa sheria zote za uchaguzi zimeweza kuzingatiwa na wapiga kura kuweza kulidhika na viongozi wote waliowachagua kwa kuwapatia idadi kubwa ya kura za NDIO kutoka kwa wapiga kura hao ambao idadi kamili ilikuwa ni 101.Yafuatayo ni majina ya viongozi wapya pamoja na vyeo vyao ndani ya SSPRA pamoja na idadi za kura walizozipata. 

MWENYEKITI - CHRISTOPHER T. NGONYANI (BAPRM 2) amepata kura 100 za NDIO na kupata kura 1 ya HAPANA,,katika nafasi hii ya Mwenyekiti alikuwa mgombea pekee. 

MAKAMU MWENYEKITI- MSEKWA B. CHEBY (BAPRM 2) amepata kura 99 za NDIO na 2 za HAPANA,katika nafasi hii alikuwa mgombea pekee. 

KATIBU MKUU-MLAY P.MZEE (BAPRM 2)amepata kura 63 zidi ya Mwema F. Kihengu ambaye amepata kura 38,hivyo basi MLAY P.MZEE ndio KATIBU MKUU mpya wa nafasi hii ambayo ilikuwa ikishikiriwa na Bw.Ngonyani ambaye kwa sasa amekuwa ndio Mwenyekiti.

KATIBU MKUU MSAIDIZI - ATHANAS MATHIAS(BAPRM 1) amepata kura 101 za NDIO. 

MWEKA HAZINA (TREASURER) - JACQUELINE P. KOWA (BAPRM 2) amepata kura 96 za NDIO na kura 4 za hapana katika nafasi hii alikuwa mgombea pekee.

 MWEKA HAZINA MSAIDIZI - SING'AMBI ATHANAS (BAPRM 1) amepata kura 96 za NDIO na kura 5 za HAPANA. 

MSEMAJI MKUU (PUBLIC RELATIONS OFFICER) AIDAN W. KAIJANANTE (BAPRM 2) amepata kura 68 zidi ya mpizani wake Bw. MBWAGA E. AMAN ambaye amepata kura 27 wakati kura 5 zikaharibika. 

MSEMAJI MSAIDIZI (ASSISTANCE PRO) - JOHN JAMES amepata kura 91 za NDIO na kura 9 za HAPANA. .
wanachama wa SSPRA wakiwa katika kikao cha pamoja kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wapya
 Makamu Mwenyekiti mstaafu Bw.Medard akitoa maelekezo mbalimbali.


Wanakamati wastaafu wakitoa maelezo mbalimbali kwa wanachama wa kawaida.

Kamati ya uhusiano wa vyombo vya habari na machapisho wakiteta nao jambo.





Makamu mwenyekiti Msekwa Cheby akijinadi mbele ya wapiga kura kabla ya uchaguzi
                                          Katibu mkuu wa SSPRA Bwana Mlay P. Mzee

Mwema F.Kihengu akimwaga sera zake mbele ya wapiga kura
                                          Katibu Mkuu msaidizi mpya  Athanas Mathias
Mweka hazina  Jacqueline P.Kowa
Msemaji mkuu (PRO) wa SSPRA Bw. Aidan W Kaijanante
Aman E. Mbwaga ambaye akijinadi mbele ya wapiga kura aweze kuwa PRO wa SSPRA






Yusufu Manning ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa SSPRA alikuwepo pia



     Picha ya pamoja baada ya uchaguzi




Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA