Taarifa ya mabadiliko ya tarehe ya kuapishwa na kuzinduliwa tume ya mabadiliko ya Katiba


TAARIFA KWA VYOMBOVYA HABARI 
MABADILIKO YA TAREHE YA KUAPISHWA NA KUZINDULIWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameamua kusogeza mbele siku na tarehe ya kuapishwa Mwenyekiti, Naibu Mwenyekiti, Wajumbe, Katibu na Naibu Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo, Jumatatu, Aprili 9, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa badala ya Mheshimiwa Rais Kikwete kuwaapisha Ijumaa ya wiki hii, Aprili 13, 2012, sasa atawaapisha saa nne asubuhi ya Jumatatu ya Aprili 30, 2012.

Taarifa ya Balozi Sefue imesema kuwa katika kufikia uamuzi wake, Mheshimiwa Rais Kikwete amezingatiamambo yafuatayo:

Moja, ni kwamba kutokana na umuhimu wa shughuli hii, yanahitajika maandalizi ya kutosha ili uzinduzi wa Tume upate hadhi inayostahili na kusiwe na muda mrefu kati ya uzinduzi na kuanza kazi. Kisheria, Tume itaanza kazi yake Mei mosi, 2012.

Pili, majukumu ambayo Tume inakabidhiwa ni makubwa sana, yanayogusa mustakabali wa Taifa na hivyokuhitaji umakini mkubwa na muda wote wa Wajumbe na wa Sekretarieti. Mheshimiwa Rais anafahamu fika kuwa aliowateua kwa sasa wanazo shughuli zao na wanahitaji muda wakujiandaa ili wakiapishwa wawe tayari kuanza kazi mara moja na kuifanya kazi hiyo kwa muda wao wote ili lengo la kuwa na Katiba Mpya ifikapo Aprili 26,2014, lifikiwe na Katiba hiyo itumike kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hivyo, Mheshimiwa Rais anatumaini kuwa walioteuliwa watatumia wiki tatu zijazo kujiandaa kwa kazi kubwa inayowasubiri.

Tatu, Mheshimiwa Rais amefahamishwa pia kuwa wapo miongoni mwa aliowateua ambao wamesafiri na asingependa kukatisha safari zao. Muda alioutoa sasa utawawezesha kurejea na kuhitimisha shughuli zao nyingine tayari kwa kuapishwa Jumatatu ya Aprili 30, 2012 na kuanza kazi yao ya Tume siku inayofuata ya Jumanne, Mei Mosi, 2012 kamailivyopangwa.

Imetolewa na:

Kurugenzi yaMawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DARES SALAAM.

9 Aprili, 2012

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA