TAKUKURU YAKAMATA MAAFSA ARDHI-MUSOMA VIJIJINI
Kutoka kwa mwakilishi wa blog hii kutoka Musomana
Shomari Binda
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
Mkoani Mara imewakamata na kuwashikilia Wajumbe wanne wa Baraza la Ardhi Kata ya
Nyakatende Wilaya ya Musoma Vijijini kwa kosa la kuomba na kupokea hongo ya
shilingi laki mbili kinyume na Sheria za Kuzuia na kupambana na
Rushwa.
Akitoa Taarifa kwa vyombo vya Habari, Naibu Mkuu wa Takukuru
Mkoani Mara Yustina Chagaka alisema kuwa waliokamaywa ni Katibu wa Baraza hilo
Morland Maijo pamoja na Malima Kitonge,Richard Rugembe na Monica Juma ambao ni
Wajumbe wa Baraza hilo.
...
Alisema kuwa Wajumbe hao waliomba kupatiwa hongo
hiyo kutokana kwa mwananchi aliyekuwa na mgogoro wa shamba uliowafikisha katika
Baraza hilo kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.
Alidai watuhumiwa hao
wakiongozwa na Katibu wa Baraza hilo waliomba kupatiwa kiasa cha shilingi laki
tano ili wagawane lakini baada ya mlalamikaji kudai kuwa hana kiasi hicho ndipo
walipomtaka awape kiasi cha shilingi laki mbili na kile kitakachobaki shilingi
laki tatu azimalizie tarehe April 16 mwaka huu ili aweze kupewa upendeleo katika
shauri lake.
"Katibu huyom pamoja na wenzake waliomba kupatiwa fedha
kiasi hicho ili wagawane, Lakini baada ya mlalamikaji kudai kuwa hana kiasi
hicho walimtaka April 3 mwka huu awapelekee kiasi cha shilingi laki
mbili,"alisema Yustina.
Yustina alisema kuwa Uchunguzi bado unaendelea
kwa watuhumiwa hao na pale utakapo kamilika watafikishwa Mahakamani ili,kuweza
kuchukuliwa hatua za kisheria na kutoa wito kwa Wananchi kuweza kushirikiana na
Taasisi hiyo kutoa taarifa za vitendo vya kama hivyo
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Mara imewakamata na kuwashikilia Wajumbe wanne wa Baraza la Ardhi Kata ya Nyakatende Wilaya ya Musoma Vijijini kwa kosa la kuomba na kupokea hongo ya shilingi laki mbili kinyume na Sheria za Kuzuia na kupambana na Rushwa.
Akitoa Taarifa kwa vyombo vya Habari, Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoani Mara Yustina Chagaka alisema kuwa waliokamaywa ni Katibu wa Baraza hilo Morland Maijo pamoja na Malima Kitonge,Richard Rugembe na Monica Juma ambao ni Wajumbe wa Baraza hilo.
...
Alisema kuwa Wajumbe hao waliomba kupatiwa hongo hiyo kutokana kwa mwananchi aliyekuwa na mgogoro wa shamba uliowafikisha katika Baraza hilo kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.
Alidai watuhumiwa hao wakiongozwa na Katibu wa Baraza hilo waliomba kupatiwa kiasa cha shilingi laki tano ili wagawane lakini baada ya mlalamikaji kudai kuwa hana kiasi hicho ndipo walipomtaka awape kiasi cha shilingi laki mbili na kile kitakachobaki shilingi laki tatu azimalizie tarehe April 16 mwaka huu ili aweze kupewa upendeleo katika shauri lake.
"Katibu huyom pamoja na wenzake waliomba kupatiwa fedha kiasi hicho ili wagawane, Lakini baada ya mlalamikaji kudai kuwa hana kiasi hicho walimtaka April 3 mwka huu awapelekee kiasi cha shilingi laki mbili,"alisema Yustina.
Yustina alisema kuwa Uchunguzi bado unaendelea kwa watuhumiwa hao na pale utakapo kamilika watafikishwa Mahakamani ili,kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria na kutoa wito kwa Wananchi kuweza kushirikiana na Taasisi hiyo kutoa taarifa za vitendo vya kama hivyo
Comments
Post a Comment