HOSPITALI YA MUSOMA YAKABILIWA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU

HOSPITALI ya mkoa wa Mara mjini Musoma bado inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa damu jambo ambalo limetajwa wakati mwingine kuchangia vifo hasa vya wanawake wajawazito na watoto.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Mara Dk Joseph Nyamagwira Amesema kupungua kwa damu katika hospitali hiyo kumetokana na mwamko mdogo wa wananchi katika kuchangia damu hiyo hivi sasa.

Amesema ingawa hospitali imekuwa ikijitahidi kuhifadhi sehemu ya damu kwa ajili kukabiliana na dharura,lakini wakati mwingine benki ya damu ya hospitali hiyo imekuwa ikiishiwa kabisa ikiwemo damu ya kundi la O jambo ambalo limekuwa likisabisha wagonjwa wa kundi hilo kupoteza maisha.

Hata hivyo Dk Nyamagwira,amesema pamoja na ndugu za wagonjwa kujitolewa kuchangia damu hiyo,lakini kutokana na magonjwa yaliopo hivi sasa damu hiyo imekuwa haitumiki kumuongezea mgonjwa wakati huo hadi ipelekwe kwenye vipimo vikubwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza ambapo zaidi ya asilimia 50 ya damu hiyo mara nyingi imekuwa ikimwagwa baada ya kubainika kuwa si salama.

Kwa sababu hiyo ametoa wito kwa taasisi za shule,vyuo,majeshi na watu binafsi kurudia zoezi kama ilivyokuwa awali kwa kujitolea kutoa damu ambayo itasadia kuokoa maisha ya watu wengine wakiwemo watoto,wanawake wajawazito na wananchi wanaopatwa na majanga ya ajali.
Taarifa hii ni kwa hisani ya Agustino mgendi mwakilishi wa blog hii kutoka Musoma.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA