JESHI la Polisi Mkoa wa Mara litatoa zawadi ya shilingi laki sita

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara litatoa zawadi ya shilingi laki sita pamoja na tuzo kwa Kikosi Kazi cha Askari wake waliokataa kupewa
Rushwa ya shilingi laki tatu baada ya kuwakamata watu wawili
wanaodaiwa kumtapeli Mwalimu mmoja shillingi Milioni tano.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Robert Boaz alisema kuwa kitendo kilichofanywa na askari hao
ni cha kuigwa na wengine ili kupunguza kashifa zisizo za msingi pamoja
kuwafanya wananchi kurudisha uaminifu ndani ya jeshi hilo.

“Askari hawa kukataa rushwa ni kitendo cha kiungwana na wanahitaji
pongezi na sisi kama Viongozi wao lazima tuwape tunzo mara mbili ya
fedha walioikataa ili kuweza kuwatia moyo askari wetu kukataa
rushwa,”alisema Boaz.

Kamanda Boaz ametoa rai kwa askari wengine kuwa wakipewa rushwa
wachukue lakini wamfikishe mtoa rushwa Polisi ili wazawadiwe mara
mbili ya fedha waliopewa.

Akielezea tukio hilo Kamanda Boaz alisema kuwa Machi 29 mwaka huu
askari hao walimkamata Said Hamis (33) ambaye alikuwa akiendesha gari
lenye namba T 317 ALR akiwa na Jackline Moses (30) wote wakazi wa
Mwanza kwa tuhuma za kumtapeli fedha kiasi cha milioni tano mwalimu
Kazia Katende (56).

“Siku hiyo ya tukio mwalimu huyo alikuwa akitoka benki kuchukua fedha
ambapo alikutana na matapeli hao na kumuambia wanataka kumuuzia madini
na aliingia katika gari la matapeli hao na kuelekea barabara ya
majita,

“Walipofika maeneo Fulani inadaiwa kuwa Mwalimu huyo alikwenda kununua
soda na aliposhuka gari liliondoka huku mkoba wake uliokuwa na hela
wakaondoka nao ndipo alipopiga simu polisi na kutaja namba za gari
hilo na ndipo polisi walianza kulisaka na kufanikiwa
kuwakamata,”alisema Kamanda Boaz.

Kamanda Boaz ametoa wito kwa wananchi na wakazi wa Mkoa huo kuacha
kununua vitu vya magendo na kuchukua taadhali na watu wanaowashawishi
kuingia katika biashara wasizozijua pamoja na kuwashawishi askari
kupokea rushwa.

habari imeandaliwa na Thomas Dominick,
Musoma.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA