UTAPELI MPYA KATIKA FOLENI ZA MAGARI WAZIDI KUSHIKA KASI JIJINI DAR
Kuna aina mpya imeingia siku hizi jijini Dar es Salaam.
Unapokua
katika yale maeneo ya foleni kali muda ya kwenda kazini ama kurudi
nyumbani, anatokea mtu kwa mbele kama anavuka na kukuonyesha ishara
yaani kama fungua vioo, na kisha anakupa ishara zaidi kua uangalie nyuma
ya gari yako (wakati huo wewe upo kwenye foleni na hivyo unazingatia
magari yanasogee ili na wewe usogee), wakati yule mtu wa mbele yako yupo
"busy" kukupa ishara mbalimbali, kumbe ile ni kukuvuruga akili.
Papohapo utasikia kitu kama kishindo kwa nyuma ya gari lako (ni mtu
kajigongesha kwenye gari yako na kujiangusha ili wadai umemgonga) kumbe
ni mwenzie yule wa mbele aliyekuwa anakupa ishara za uongo na kweli.
Wote ni matapeli.
Kitendo hiki kinafanyika haraka sana, yaani
kufumba nakufumbua, yule mtu anapojigongesha tu kwenye gari, wenzake
watatokeza pasipojulikana na kulizunguka gari.
Utakapofanya
uungwana wa kufungua vioo vyako au kushuka toka kwenye gari lako, ndipo
kosa unapokuwa umelitenda kwani unawaachia mwanya wa wao kukuliza kwani
kwa "speed" ya ajabu mwenye kuchukua simu, pochi ama briefcase yako au
chochote cha thamani kilicho katika gari lako, watafanya hivyo "fasta"
sana. Watakuwa wanakuzunguka na kusema ''umeua, umeuaa....'' ili
kukutia hofu, na wewe utastuka na kumjali yule jamaa alieanguka pale
chini. Baada ya dakika chache tu, unajikuta umebaki wewe na wengine wote
wamekimbia, salama yako wasikupige kwani wakati mwingine wanadiriki
kukupiga ili kukuogofya na ujitetee.
Comments
Post a Comment