HABARI ZA LEO KUTOKA MUSOMA


KUTOKA KWA MWANDISHI AUGUSTINO MGENDI
MUSOMA

JESHI LA POLISI MKOANI MARA LINAWASHIKILIA VIJANA WANNE KUTOKA MWISENGE NA BARABARA YA MAJITA KWA TUHUMA ZA KUMCHOMA KISU MWENZAO MMOJA BAADA YA KUTOKEA KUTOELEWANA BAINA YAO

AKIONGEA NA KITUO HIKI LEO KAIMU KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA MARA SSP EMANUEL LUKULA AMESEMA KUWA VIJANA HAO WAKO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI KWA AJILI YA UCHUNGUZI ZAIDI ILI KUBAINI CHANZO CHA TUKIO HILO
...

KAIMU KAMANDA WA JESHI LA POLISI LUKULA AMETHIBITISHA KUTOKEA KWATUKIO HILO NA PIA KAIMU KAMANDA HUYO AMESEMA KUWA TUKIO JINGINE LIMETOKEA MAENEO YA KOTRA MANISPAA YA MUSOMA AMBAPO MAJAMBAZI WALIVAMIA NA KUWAKATA MAPANGA WALINZI WAWILI NA KISHA KUWAFUNGA KAMBA NA BAADA YA HAPO WAKAIBA POMBE KALI ZENYE THAMANI YA SHILINGI LAKI 2 NA ELFU 20

AMESEMA KUWA TUKIO HILO LIMETOKEA SIKU YA JUMAMOSI MAJIRA YA SAA SABA USIKU AMBAPO WASHUKIWA WA TUKIO HILO BADO HAWAJATIWA MBARONI

KUHUSU SIKUKUU YA PASAKA KAIMU KAMANDA LUKULA AMESEMA KUWA ILIKUWA SALAMA NA HAKUKUWA NA TUKIO LOLOTE BAYA LILILOTOKEA

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

SERENGETI

WAKATI WATANZANIA WOTE WALIOKO MIJINI NA VIJIJINI WAKIENDELEA KULIANA MFUMUKO WA BEI ZA VYAKULA NA BIDHAA TOFAUTI HALI AMBAYO IMEPELEKEA BAADHI YA FAMILIA KUSHINDWA KULA MILO MITATU KWA SIKU BEI YA VYAKULA KATIKA SOKO LA MUGUMU WILAYANI SERENGETI MKOA WA MARA IMESHUKA KWA KIWANGO KIKUBWA.

WAKIONGEA NA MWANDISHI WA HABARI HIZI VIONGOZI WA SOKO KUU LA MUGUMUNA BAADHI YA WANANCHI WALIKIRI KUSHUKA KWA BEI YA NAFAKA NA HATAMAKUSANYO YA USHURU YAMEONGEZEKA IKIWA NI TOFAUTI NA AWALI AMBAPO MAKUSANYO YA USHURU YALIPUNGUA KWA KUWA WAFANYABIASHARA WALIPUNGUA .
.
MWENYEKITI WA SOKO HILO BWANA SIMIONI MAKURU AMESEMA KUWA KWA SASABEI YA BIDHAA MBALIMBALI IKIWEMO CHAKULA IMESHUKA KATI YA ASILIMIA 25HADI 10 KULINGANISHA NA BEI YA AWALI ILIYODUMU KWA ASILIMIA 100 YABIDHAA HUSIKA NA KUPELEKEA MAISHA YA MTANZANIA WA KIPATO CHA CHINIKUSHINDWA KUMUDU GHARAMA ZA MAISHA.

NAO BAADHI YA WANANCHI WAMEDAI KUWA BEI YA MAZAO KAMA MAHINDI
,MTAMA,MAHARAGE NA MUHOGO AMBAYO HUTUMIWA KILA SIKU KAMA CHAKULA
YALIPANDA BEI NA FAMILIA NYINGI ZILILAZIMIKA KULA MLO MMOJA KWA SIKU.

KATIKA SOKO HILO KWASASA MAHINDI YAMESHUKA KUTOKA TSH, 12,000= HADI TSH, 7,000= UDAGA KUTOKA TSH, 7,000 HADI 4,500=KWA DEBE.,NA HUENDA BEI IKAZIDI KUSHUKA KWA KUWA MVUA INAENDELEA KUNYESHA NA KUNA MATUMAINI YA KUVUNA MSIMU MFUPI.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA