'NI NASARI NI CHADEMA ARUMERU MASHARIKI'

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Kushoto ni Mkazi wa Arumeru Mkoani Arusha, akipiga kura katika kituo cha Ngaresero, uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, jana. Picha na Edwin Mjwahuzi wa gazeti la Mwananchi.
 Matokeo ya uchaguzi wa Ubunge wilayani Arumeru Mashariki yametangazwa rasmi asubuhi ya leo mara baada ya zoezi la kuhakiki uhesabu kura lililochukuwa muda mrefu kukamilika na matokeo yakimpa ushindi mgombea wa CHADEMA bwana Nasari Joshua;

KURA HALALI:
60038
ZILIZOKATALIWA:
661
Wagombea:
Mazengo Adam AFP
139

Charles Msuya UDP
18

TLP
18

Kirita Shauri Moyo
22

Hamisi Kiemi
35

Mohammed DP
77

Sumari Solomon CCM
26757

Nassari Joshua CHADEMA
32,972

Huu ni uchaguzi wa kwanza mdogo kwa CHADEMA kushinda katika jimbo lililokuwa likishikiliwa na CCM na uchaguzi wa pili kwa chama hicho cha upinzani, kushinda katika uchaguzi mdogo baada ya ule uliofanyika katika Jimbo la Tarime, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Wangwe.

CHADEMA YAFANIKIWA KUTETEA KATA YAKE KIRUMBA MWANZA

Matokeo ya uchaguzi kiti cha udiwani yametangazwa rasmi jioni ya leo yakimpa ushindi mgombea udiwani kupitia tiketi ya CHADEMA Bahati Kahungu kwa tofauti ya kura 807 kwa mgombea aliyekuwa akichuana naye kwa kasi Jackson Robert 'Masamaki' wa CCM.
Vituo vyote vilimaliza majumuisho yake mapema hivyo zoezi lililokuwa limebakia hadi kufikia saa moja jioni ilikuwa ni kufanya majumuisho ya vituo vyote kisha matokeo yapate kutangazwa, yote yakijiri wafuasi wa CHADEMA walikuwa wakiimba huku wakizunguka viwanja vya Furahisha kusherehekea matokeo ya vituo vingine.
Jeshi la polisi lilijizatiti vilivyo katika suala la ulinzi.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe aliwasili viwanjani hapo kutuliza wafuasi wa chama hicho kujiepusha na vurugu kwani haki imezingatiwa.
Zito Kabwe ilimbidi kutumia kipaza sauti kuhamasisha utulivu kwani kulikuwa na kila dalili za machafuko kutokea kwa kila mmoja kuwa na imani yake dakika chache baadaye matokeo yalitangazwa na Afisa mtendaji wa kata ya Kirumba Aloyce Mkono:
CHADEMA kura 2938
CCM kura 2131
CUF kura 184
UDP kura 7
NCCR kura 0
Mara baada ya matokeo hayo kutangazwa hali ya utulivu ilitawala watu wakiamuriwa kuondoka kwenye eneo hilo.
Askari akiamuru watu kufungua njia ili masanduku ya kura yapakiwe kwenda kuhifadhiwa.
Full ulinzi.
Masanduku ya kura yakipakiwa garini.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA