MAPA TRADERS WATOA PUNGUZO LA PASAKA

Kampuni ya Mapa Traders Company Limited ya Mjini Musoma imeingiza bidhaa mbalimbali za maofisini na Majumbani na kutoa punguzo la asilimia 20 ikiwa ni katika kusherehekea sikukuu ya Pasaka.
...
Akizungumza na BINDA NEWS katika Show Room ya Kampuni hiyo iliyopo katika barabara ya Nyerere karibu na Benki ya NMB,Afisa Mauzo wa Kampuni hiyo Golio Muhele amesemakuwa wametoa punguzo hilo ili kuwawezesha wateja wao kupata bidhaa mbalimbali na kusherehekea vyema sikukuu ya Pasaka.

Amesema kuwa kuna bidhaa nyingi ambazo zimeingia kutoka nje ya Nchi zenye viwango vya hali ya juu hivyo kila mmoja atakayepata nafasi yakutembelea katika Ofisi zao hawezi kutoka bure kwani kuna mahitaji ya kila aina.



Golio amesema kuwa baadhi ya bidhaa ambazo zuimengia ni pamoja na magari,pikipiki,baiskel,majokofu (friji),generator,redio,matairi ya magari,viti pamoja na meza za kisasa na bidhaa nyingine nyingi ambazo zote zina punguzo la asilimia 20.

Afisa mauzo huyo wa Mapa Traders ameongeza kuwa kwa wale watumiaji wa Gase majumbani,wameingiza mitungi ya Gase ya ORXY yenye ujazo tofauti ambayo pia wameitolea punguzo ambapo Gas ya KG 6 uhuzwa kwa shilingi 24,000/=,KG 15 uhuzwa kwa shilingi 58,000/= na KG 38 uhuzwa kwa shilingi 14,7000/=.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mapinduzi Muhele (MAPA) amewataka wakazi wote wa Manispaa ya Musoma na Mkoa wa Mara kwa ujumla kutembelea katika SHOW ROOM yao ili wapate kujionea bidhaa mbalimbali zilizopo na kufaidika na punguzo lililopo kwani kwa wale waliopata bahati ya kutembelea wamejionea.
HABARI KUTOKA SHOMARI BINDA 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA