TBL WAFANYA UZINDUZI WA CHUPA MPYA YA BALIMI MKOANI MARA

Kampuni ya Bia Tanzania TBL leo watafanya uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya Balimi ikiwa ni katika kuiweka katika muonekano kama zilivyo Bia nyingine za kampuni hiyo ikiwa na shingo ndefu maarufu kama "mwanamke nyonga".

Akizungumza na mwakilishi wa blog hii kutoka mkoani Mara Bw.Shomari Binda, meneja mauzo wa kampuni hiyo Mkoani Mara Polycalipo Makunja amesema kuwa maandalizi yote kuhusiana na uzinduzi huo yamekamilika ikiwemi kuwasili kwa timu nzima ya uongozi wa TBL kanda kutoka mkoani Mwanza.

Poly amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa bawalo la Magereza kuanzia majira ya saa 1 usiku huku kukiwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Mwanza pamoja na musoma huku wakiongozwa na bendi ya Musoma jazz.

Amesema kuwa muonekano wa chupa mpya ya Balimi hautabadilisha ladha ya kinywaji hicho kwani ladha itabaki ile ile iliyozoeleka kwa wateja wa Bia hiyo ambayo ni maalum kwa wakazi wa kanda ya ziwa.

Meneja mauzo huyo wa TBL mkoani Mara amedai kuwa katika kushuhudia uzinduzi huo kutakuwa hakuna kiingilio chochote na kuwataka wadau wote kufika katika ukumbi wa bwalo la Magereza kwa kuburudika na bidhaa za TBL kwani licha ya Balimi kutakuwa na huduma ya vinywaji vingine vinavyozalishwa na kampuni hiyo.

"Hakutakuwa na nafasi ya kunyweka kwa mnyama au Bia yeyote tofauti na zinazozalishwa na TBL kwani siku ya leo ni siku ya Balimi na siku maalum ya TBL katika ukumbi wa bwalo la Magereza",alisema Poly.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA