GODBLESS LEMA APOTEZA NAFASI YAKE YA UBUNGE

Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini 
(Chadema), Godbless Lema
Mahakama ya mkoa wa jijini Arusha imemvua ubunge aliyekuwa mbunge wa Arusha Godbless Lema asubuhi hii habari zilizotufikia zinasema uamuzi huo umetokana na kesi ya kupinga matokeo iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Godbless Lema iliyokuwa ikiendelea mkoani humo.

*******
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia CHADEMA, amepoteza kiti hicho kwa kuenguliwa na Mahakama katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kupinga ubunge wake.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Agness Mollel, Mussa Mkanga na Happy Kivuyo ambao walikuwa wanamtuhumu Mbunge huyo kwa kutoa kauli za udhalilishaji, matusi na kashifa kwa aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dkt. Batilda Buriani.

Hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji, Gabriel Rwakibarila.Katika hukumu hiyo, Lema hakuondolewa haki ya kugombea ubunge huo kwa kuwa kosa lililomtia hatiani ni matumizi mabaya ya lugha tofauti na ilivyodhaniwa kuwa ni vitendo vya rushwa. Uamuzi wa kugombea ama kutokugombea kiti hicho tena utatokana na maamuzi yake mwenyewe na ridhaa ya chama chake ikiwa kitamteua na kumpitisha kugombea.

Taarifa za watu wa karibu zinasema kuwa Lema hatakata rufaa mahakamani juu ya hukumu ya kesi hiyo, bali atakata rufaa kupitia kura ya wananchi wa Arusha Mjini wakati wa kugombea kiti hicho. 
 
Hivyo tutarajie uchaguzi mpya ndani ya siku 90. Tanzania, nchi ya uchaguzi kila uchao...!

Kweli tunahitaji Katiba Mpya yenye kukidhi haja na inayoendana na wakati.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA