JESHI la Magereza limefanikiwa kumdhibiti Mahabusu wa Kesi ya dawa za kulevya ambaye ni Raia wa Sieralioni, Abdul Koroma (33) asitoroke chini ya Ulinzi wa Askari Magereza ndani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa kumtwanga risasi na kumuua papo hapo! Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, baadhi ya wanausalama waliopangwa kulinda usalama Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa kuwa wao siyo wasemaji, walisema mtuhumiwa alikuwa anashitakiwa kwa makosa ya kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 1,229, zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 61. Kesi yake ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema. Walisema asubuhi marehemu huyo, ambaye ni mahabusu, aliletwa mahakamani na askari magereza akiwa na mahabusu wenzake na kisha kufikishwa katika mahabusu ya mahakama hiyo, baadae mtuhumiwa aliomba apelekwe chooni kujisadia, lakini ghafla akaanza jaribio la kuparamia ukuta ili akim...