FUMANIZI LA X-MASS UMELIONA? PITA HAPA

Stori: Deogratius Mongela na Chande Abdallah
Shabaash! Mwanamke mmoja, mkazi wa Mikocheni A, Dar, Catherine Kayombo ‘Catty’ anadai kumfumania mumewe aliyemtaja kwa jina la Excavery Kayombo akiwa na mchepuko alioutaja kwa jina la Mariamu Kauke ‘Mamuu’ ndani ya Sikukuu ya Krismasi ‘X-Mas’, Ijumaa Wikienda limesheheni.
Mchepuko unaojulikana kama Mariamu Kauke ‘Mamuu’ ukiwa katika kitanda cha mume wa mtu.
MAJIRANI WAPENYEZA UBUYU
Tukio hilo la aina yake lilitokea majira ya mchana maeneo ya Mikocheni A ambapo Catty anayedai kupigwa na mumewe na kwenda kwao, alipata taarifa (ubuyu) kutoka kwa majirani kuwa mumewe ameingiza mwanamke nyumbani kwake na wanajiachia na kujimwayamwaya kila mahali ndani kama kumbikumbi.

Mchepuko ukikemea kupigwa picha dirishani.
Baada ya kupata taarifa hizo, Catty alikwenda nyumbani kwake kisha akamfuatilia mumewe na mwanamke huyo hatua kwa hatua kupitia dirisha la chumba chao ‘kwa baba na mama’.
Mume wa mtu, Excavery Kayombo akiwa na mchepuko huo.
FULL KUJIACHIA
Catty alidai kwamba alimshuhudia mwanamke huyo akiwa amejiachia na kujimwayamwaya kwenye kitanda chake akiwa na kijitaulo huku mumewe akiingia bafuni kuoga baada ya kufanya yao.
Alisema baada ya kujionea kila kitu laivu, Catty aliwafotoa picha kadhaa kwa kutumia kilongalonga chake cha kiganjani ambapo mchepuko huo ulimshtukia na kumuita mume wa Catty ambaye alikuwa bafuni akimwambia kuwa mkewe amefika huku akiwa hana wasiwasi.

Mke halali wa Bw. Excavery Kayombo, Catherine Kayombo ‘Catty’.
BILA WASIWASI
Catty alidai kwamba mwanaume huyo alitoka bafuni bila kujali picha alizokuwa akipigwa na mkewe kupitia dirishani na kumwambia kuwa hata akipiga na kuzipeleka magazetini yeye hajali hata kidogo. Akafunguka kuwa ameamua kuishi na Mamuu na atamuoa ‘soon’.
Mchepuko ulionaswa, Mariamu Kauke ‘Mamuu’.
Kama hiyo haitoshi, Ijumaa Wikienda lilipofika eneo la tukio lilishuhudia mambo ambapo Catty ambaye amezaa na mumewe huyo watoto wanne, aliwaambia waandishi wetu kuwa anachotaka kwa sasa kwa mwanaume huyo ni talaka tu.
Paparazi akipata undani wa habari kutoka kwa Catherine Kayombo ‘Catty’(mke wa Bw. Excavery Kayombo) .
Katika hali ya kushangaza, mumewe huyo alimwacha Catty nyumbani hapo na kuondoka na mchepuko wake kila mmoja akiwa na gari lake. Mume alikuwa na gari lake aina ya Toyota Prado na mwanamke alikuwa na gari lake aina ya Toyota Mazda.
Gari la Bw. Excavery Kayombo likiwa eneo la tukio.
WAKUTANA BAA
Baada ya Catty kuondoka nyumbani hapo akiwa na majirani zake, walikwenda kwenye baa moja iliyopo jirani na nyumbani kwake iitwayo Five Ways ambapo walimkuta tena mumewe huyo akiwa na mchepuko wake wakinywa moja moto, moja baridi bila wasiwasi wowote.

Waandishi wetu walipofika eneo la tukio walimshuhudia mwanaume huyo akikimbilia kwenye gari lake huku mchepuko wake ukiwa kwenye gari la nyuma wote wakiondoka ambapo taarifa za kiintelijensia zilidai kuwa walikuwa wakirudi tena nyumbani kwake.
Gari la mchepuko likiwa eneo la tukio.
BOFYA HAPA KUMSIKIA MWENYE MUME
“Yaani hamuwezi kuamini huyo mwanaume alivyonifanyia! Eti ananijibu bila aibu kwamba atamuoa huyo mwanamke wake. Mimi sina tatizo nimeomba talaka yangu anipatie nijue ustaarabu wangu maana tabia yake hii imenichosha, nimemvumilia sana,” alisema Catty akiwa ‘amepaniki’.
Bw. Excavery Kayombo akiwa na mchepuko wake Kwenye baa.
Alipotafutwa mwanamke anayetembea na mume wa Catty, Mamuu alisema: “Nilipofika ndani ya nyumba sikumwona mwanamke yeyote. Ninavyojua watu hawa wameachana ndiyo maana nimeamua kukaa hapa, mimi siyo mtu nisiyekuwa na akili najitambua.”
Kwa upande wake mwanaume huyo hakutaka kuzungumza na wanahabari wetu zaidi ya kukimbilia kwenye gari na kujifungia.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA