WATANZANIA WASHINDA MASHINDANO YA KUCHEZA MUZIKI KENYA

Washindi wa shindano la kucheza muziki, The Band wakionyesha mfano wa hundi ya shilingi milioni 1 ya Kenya.
Washindi wa Sakata Mashariki 2014, The Band kutoka Kenya wakipewa mfano wa hundi kama zawadi
Kundi la DSI likiwa katika mchuano huo jana usiku.
Washindi wa pili kundi la IDU kutoka Uganda likiwa katika kucheza.
Kundi la kucheza muziki lililokuwa likiwakilisha Tanzania, T-Africa likiwa katika pozi kusubiri matokeo.
Majaji wakifuatilia shindano hilo la kucheza muziki.
Kundi la Shakers likimaliza shoo kwa mbwembwe.
HATIMAYE Watanzania ambao wana vipaji  vya kucheza muziki, T-Africa wametutoa kimasomaso kwa kuchukuwa nafasi ya tatu katika shindano kubwa la kucheza muziki lijulikanalo kama Sakata Mashariki linaloshirikisha nchi tatu Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda.
Katika fainali hizo zilizofanyika jana saa nne usiku moja kwa moja kupitia Runinga ya Citizen TV ya Kenya, kundi la The Band kutoka Kenya liliibuka kidedea ikiwa ni mara yao ya tatu kushiriki na kuambulia patupu kila mara ambapo jana usiku lilifanikiwa kujizolea kiasi cha milioni 1 za Kenya (sawa na shilingi mil. 18  za Kitanzania) wakati washindi wa pili wakiwa kundi la IDU la Uganda ambao walijizolea kiasi cha shilingi za Kikenya 300,000 (sawa na shilingi mil. 5,400,000 za Kitanzania) na ushindi wa tatu ulienda kwa kundi kutoka Tanzania la T-Africa waliojizolea kiasi cha shilingi 200,000 za Kenya (sawa na shilingi mil. 3,600,000 za Kitanzania).
Makundi mengine yaliokuwa yameshiriki ni pamoja na Wakali Sisi, Tatanisha, Al Pacino, DSI, Shakers, Limbo na mengine kibao yote kutoka Afrika Mashariki.

CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA