HII NDIO KAULI YA PRO.TIBAIJUKA BAADA YA RAIS KUTENGUA UTEUZI WAKE

[Baadhi ya] Wananchi mkoani Kagera wamepinga uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi na kuwaweka kiporo viongozi wengine walioshiri kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.

Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya mkoa huo akiwemo Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kagera, Hamim Mahamoud amepongeza uamuzi wa Rais alioutoa jana kwa kumuondoa kiongozi huyo.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Manispaa ya Bukoba, Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahihi. Amemtaka Rais kuwafahamisha Watanzania ni lini pesa za Escrow zitarudishwa katika akaunti hiyo. Akahoji ikiwa kuwaondoa viongozi hao madarakani ndiyo suluhisho la kwamba pesa hizo hazirudishi?

Naye Profesa Anna Tibaijuka amesema baada ya Rais kumuondoa katika nafasi yake aliyokuwa nayo, sasa amerudi jimboni kwake kwa ajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafisi ya kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na kwamba, pesa hizo alizopewa na Rugemalila zilikuwa za kusaidia shule na alipewa kama zawadi bila kujua kama pesa hizo zilitoka katika akaunti ya Tegeta Escrow, ndiyo maana hakutaka kujiuzulu.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA