MAKALA: MATATIZO YA NDOA NA UMRI

MWANAUME MKUBWA ANAYEOA MSICHANA MDOGO
Imekuwa ni kawaida katika jamii za kiafrika wanaume wenye umri mkubwa sana kuoa wasichana wenye umri mdogo ambao wanaweza hata kuwazaa.Katika hili imekuwa ni kama fashion kwa wasichana kiasi wamekosa hata zile haya walizokuwa nazo wazazi wetu enzi za zamani.

Wasichana wengi wametokea kujidumbukiza kuolewa na mababa wakubwa sana hari si kuwa wanapenda kuolewa na wazee waliowazidi umri kwa kiasi kikubwa.Wachache kati yao wanapenda kuolewa na watu wazima na wengi kati ya hao hawapendi kabisa ndoa za namna hiyo.

SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA WASICHANA WADOGO WALAZIMIKE KUOLEWA NA WANAUME WATU WAZIMA

Moja ya sababu ambazo inapeleka wasichana wadogo kukubali kuolewa na wanaume wakubwa waliowazidi umri sana ni Pesa,Sifa za majina ya wanaume jijini au nchi walizopo,Umasikini wa familia walizotoka.hapo zamani wanawake wengi waliolewa na wanaume kwa kukubali mapenzi ya dhati na kuzingatia maadili mazuri ya ndoa.hawakuangalia suala la pesa au kuolewa na watu wenye majina makubwamakubwa walipenda sana wanaume waaminifu na wachapa kazi, wao pesa ilikuwa ni majaaliwa ya Mungu.

Wasichana wa kileo wamekuwa na tamaa za harakaharaka kimasha na kutopenda kabisa kwenda kwenye ndoa yenye mashaka au dhiki za maisha.
Kila msichana amekuwa akimtamani mwanaume yeyote yule mwenye pesa ili mradi akafaidi maisha ya kileo na uhakika wa kila anachokiona kipya akipate.

Mabinti wa kisasa hawapendi kujituma kama wale wa zamani ambao walikuwa wakitwanga,wakichota maji,wakifua na hata kulima na kusaidia mifugo pamoja na waume zao,siku hizi mtoto wa kike unamkuta hataki kucha zake zikatike kwa kufua au kumsaidia mumewe kufua.

Wengi wa wasichana wamekuwa na kasumba ya kuolewa na mwanaume yoyote yule mwenye pesa ili kuondokana na umasikini wa familia zao bila kufanya uchunguzi wowote ambao uleta hathari katika ndoa zao.

MATATIZO YA NDOA NA UMRI (ATHARI)
Uchunguzi nilioufanya katika wana ndoa wengi toka jamii za kiafrika wanapatwa na matatizo mengi ndani ya ndoa zao muda mchache tu mara ya kuingia katika ndoa na watu wasiowafanyia uchunguzi wa kina kabla ya kukubali kuolewa.

Tukianzia kwa upande wa wasichana ambao wamekuwa wakuimizwa sana na wanaume waliokubali kuolewa nao kwa kufuata pesa ili kujikomboa kutoka hari fulani ya kiwango cha chini kimaisha na kwenda huko kwa matajiri wakifikiri watapata ahueni kwao.Au  wale waliopenda kuolewa kwa kufuata umaarufu wa wanaume wenye majina makubwa(Famours People).


Wanaume wengi wanawalaghai wasichana wadogo kwa ahadi bandia [fake] pindi wanapotaka kuwa nao,wengine uwapa magari kama zuga toto ili wakubali kuolewa nao,wengine uwadanganya kwa kuwajengea nyumba.

(Athari namba Moja)

Wengi wa wasichana wamezikwa kwa ukimwi kutokana na tamaa za kuolewa na wanaume wakubwa hari ya kutaka maisha mazuri kwa kuona nikiolewa na mwenye pesa nitaneemeka kimaisha.

(Athari namba mbili)

Wengine wameathirika kisaikolojia kwa kulazimika kukubali kuwa wake wenza hari ya kuwa hawakutarajia haya mwanzoni.

(Athari namba Tatu)
Kadhalika wasichana wengi wamekuwa wakiteseka na ndoa zao kwa kutopata mapenzi waliyotarajia na hii inatokana na wanaume wengi wenye pesa kukosa muda wa kukaa na wake zao kutokana na shughuli za kazi zao zinavyowabana.

(Athari namba Nne)
Wengi wa wanaume wenye pesa ni wahuni kiasi kwamba wanawatesa wasichana wengi waliojiingiza bila kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuolewa nao.Na matokeo yake wanabaki na simanzi kila kukicha kwa kushindwa kuondoka kwenye ndoa wakifikiri watachekwa na wenzao au jamii inayomzunguka kutokana na sifa walizozifuata wakizani watazikosa maishani…

Kwa leo tuishia hapa mpaka juma lijalo

Na

Mwandishi wako Maganga One
magangaone@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA