NDOA ZA MIKEKA TISHIO ZANZIBAR

Kuongezeka kwa ndoa za mikeka
kumesababisha kuongezeka kwa talaka katika
Mahakama Kuu Z’bar ambapo mwanaharakati
wa Chama cha Wanahabari, Amina Talib
amesema ndoa hizo ambazo zinafahamika pia kama ndoa za kukamatiwa zinaharibu mfumo
mzima wa maisha.

Amina alisema katika Ripoti zilizotolewa na chama hicho, Mahakama za kadhi ambazo
zimekuwa na majukumu ya kusikiliza kesi za ndoa na mirathi zimeelemewa na idadi kubwa
ya maombi ya talaka huku watendaji wa Mahakama hiyo wakilaumu wananchi
kutochukua hatua yoyote kunusuru hali hiyo.

Wazazi wametakiwa kuwalea watoto wao kwa maadili ili kukwepa vitendo vya ushawishi wa
kuingia katika uhusiano wa kimapenzi kabla ya
umri.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA