MASHABIKI WAHOJI JUU YA VIDEO YA "MWANA" YA ALI KIBA MBONA HAIENDANI NA STORY YA WIMBO?

Ali Kiba ambaye yuko chini ya usimamizi wa Rockstar400 ametoa video ya single yake mpya ya  "Mwana" iliyotengenezwa na kampuni ya GodFather productions, hii ni single ya kwanza ikiitambulisha album yake ya tatu. Video hii mpaka hivi sasa imefikisha watizamaji 51,447 tangu kuwekwa jana katika account ya Ali kiba ya Youtube.
Mashabiki wa muziki wa bongo fleva wamekuwa katika mabishano makubwa kuanzia jana baada ya kuanza kuitizama video hiyo kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo whatsapp, wanahoji je video mbona haiendani na maudhui (content) ya nyimbo?. Mashabiki wanahoji je mbona mwana Dar es salaam anayezungumzia hajaonekana hata scene moja mpaka video inaisha.Penye kukosoa pia kuna pongezi kwa kawaida watu wote hawawezi kuwa na mtizamo mmoja, wapo mashabiki wengine wameisifia video hii kwa ilivyoandaliwa kwani imekuwa ya kiutofauti wakiifananisha na video ya Chris Brown "Loyal" ambayo story yake iko tofauti na kinachozungumziwa kwenye audio.
Kuna mengi ya kujiuliza, kwani video ya muziki inapotengenezwa ni lazima story iendane? Yawezekana Ali kiba alikuwa ana idea tofauti ya kufanya mtu aumize kichwa kwanza sio kufikilia kile kile mtu ambacho anafikiria kiwe na kuondoa ladha ya wimbo na kufanya mtazamaji ajue video utakavyoanza na kuishia kama movie za bongo movie, Yawezekana hii ni suprise kwa mashabiki kwamba video sio lazima ifanane na kinachozungumziwa yale sio maigizo. Quality ya video iko sawa wengi wanapongeza lakini utata umejitokeza hapo kwenye story. Je wewe una mawazo yapi juu ya video hii?
Hizi ni baadhi ya screenshots za  comments kutoka kwa washabiki wakijibizana.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA