MAAJABU MWANAUME APATA SIKU KAMA WANAWAKE

Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
MAAJABU! Ndivyo unavyoweza kusema unapokutana na mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina  la Frank Kalamu (53) mkazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam, aliyetoa ushuhuda wa kufunga mwaka kwamba kwa zaidi ya miaka miwili, alikuwa akipata siku zake kama ilivyo kwa wanawake, ingawa yeye ni kupitia njia ya haja kubwa.
Frank Kalamu akiombewa kanisani.
Akitoa ushuhuda huo ndani ya Kanisa la The Revelation lililopo Buza-Kipera Desemba 21 mwaka huu, Frank alidai amepata mateso hayo kwa muda mrefu huku akizunguka kwa waganga na madaktari wengi bila mafanikio, mbaya zaidi, kwa kipindi chote hicho ameshindwa kushiriki tendo la ndoa na mkewe.
Akizungumza na waandishi wetu nje ya kanisa, Frank alisema awali alikuwa mzima lakini ghafla alianza kwa kukosa hamu ya kushiriki tendo na mkewe, ingawa alipojaribu kuchepuka, alimudu vyema kazi hiyo.
“Baadaye dalili zilizidi kuongezeka, nikajikuta nikipata maumivu chini ya kitovu na kuanza kutoka damu kila mwezi hasa nikiwa najisaidia haja kubwa, hali hiyo huambatana na kutoka nyama sehemu za haja kubwa.
...Frank Kalamu akizidi kupokea upako.
“Nikawa nikijisaidia kitu kama utumbo unatoka, huku damu zikitoka pia, siku nyingine japokuwa ‘sikubleed’ lakini nyama hiyo ilitoka na nikawa nairudishia kwa ndani,” alisema Frank  kwa uchungu na kuongeza kuwa alianza kuhangaika kwa waganga mbalimbali bila msaada wowote.
Baada ya kuona anamaliza fedha bila kupata nafuu, Frank aliamua kutafuta huduma ya kiroho ambapo akiwa kanisani hapo, Nabii Yaspi alimwambia kuwa alikuwa amerogwa na mtu aliyemtaja kwa jina la Saidi, ambaye mgonjwa huyo alimtambua kama rafiki yake wa zamani aliyewahi kumhisi kuwa alitembea na mchumba wake.
...akitoa ushuhuda wake.
“Nabii aliponiambia kuwa ni Saidi aliyeniroga, picha ya rafiki yangu ilikuja kichwani, kila mara alinihisi natembea na mchumba wake. Nadhani aliniroga kwa sababu hiyo si nyingine,” alisema mtu huyo ambaye pia alidai kufuatia huduma ya maombezi anayoipata, anaanza kuona dalili za mabadiliko ya hali yake.



chanzo:global publishers

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA