HAPPY BIRTHDAY TANZANIA BARA (TANGANYIKA)

Leo imetimia miaka 53 tangu Tanganyika (Tanzania Bara) kupata uhuru kutoka kwa utawala wa kikoroni uliokuwa ukiongozwa na Waingereza.

Katika miaka hii 53 changamoto bado ni nyingi sana hasa katika swala la maendeleo kwa ujumla, miaka 53 ni mingi sana, serikali iliyopo madarakani bado inadeni kubwa sana kwa wananchi wake ambao wanakufa hospitalini bila kupata dawa, kushindwa gharama za matibabu, kukosa hata mlo mmoja kwa siku, tatizo la maji safi, mapigano ya kugombania ardhi kati ya wawekezaji na wananchi.

Miundo mbinu bado ni tatizo kwa taifa, Elimu inazidi kudidimia kila kukicha watoto wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika tunaelekea wapi? sera ya nchi iko wapi ambayo inatakiwa kuwa dira ya kutuongoza? Serikali bado ina deni kwa wananchi.

Amani twajivunia kila siku lakini ipo siku yaweza kutoweka kwa sababu ya waru kukata tamaa ya maisha huku wakiona viongozi wakiishi maisha kama wako peponi na familia zao huku wananchi wakikosa mahitaji makuu matatu yaani chakula, malazi na nguo.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA