NYALANDU AJITOSA RASMI MBIO ZA URAIS KUPITIA CCM 2015
Na Gasper Andrew, Mwananchi
WAZIRI wa maliasili na utalii na mbunge
wa jimbo la Singida kaskazini(CCM) ,Lazaro Samwel Nyalandu,ametangaza
rasmi nia ya kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika mwakani.
Nyalandu ametangaza nia hiyo leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ilongero Jimbo la Singida kaskazini.
Alisema baada ya kutafakari kwa muda mrefu na
kujikagua kwa kina,ameona anao uwezo wa kutosha wa kuweza kupokea kijiti
kutoka kwa rais anayemaliza muda wake mwakani kwa mujibu wa katiba.
“Kujikagua huko ni pamoja na kutafakari jinsi
alivyoweza kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM katika vipindi vitatu
(miaka 15) akiwa mbunge wa jimbo la Singida kaskazini.Katika kipindi
hicho cha ubunge,nimeweza kutumia zaidi ya shilingi bilioni mbili katika
kufanikisha kuchangia miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali
zikiwemo za afya,maji na barabara”,alisema Nyalandu.
Alisema wakati ukifika,Watanzania kutoka sehemu
mbalimbali za nchi wakiongozwa na wakazi wengi wa kutoka jimbo la
Singida kaskazini,kwenda Dodoma kuchukua fomu za kuwania urais.
“Watanzania waliokwisha onyesha nia ya kuwania
urais mwakani,nawaomba sote tuonyeshe kazi tulizozifanya katika
kuwahudumia Watanzania,ili waweze kutupima vizuri waweze kujijengea
mazingira mazuri ya kuchangua rais atakayewafaa kwa kuwaletea maendeleo
endelevu”,alisema.
Nyalandu alisema kuwa anakishukuru Chama Cha
Mapinduzi,kwa maandalizi yake mazuri ya kuhakikisha chama kinapata
mwanaCCM safi,mwadilifu na mchapa kazi atakayepeperusha bendera ya chama
katika kinyang’anyiro cha kuwania urais mwakani.
CHANZO:mwananchi.co.tz
CHANZO:mwananchi.co.tz
Comments
Post a Comment