WIZI WA MTANDAO UNAVYOZIGHARIMU BENKI DUNIANI
Zile nyakati za wizi wa kutumia bunduki, mapanga au visu sasa zimepitwa na wakati, badala yake, wahalifu sasa wanatumia njia ya mtandao.
Mapinduzi ya sayansi na teknolojia licha ya kuwa na manufaa chekwa, lakini katika miaka ya karibuni teknolojia hiyo imegeuka shubiri kwa watumiaji.
Matukio ya wizi kwa njia ya mtandao yameendelea kuripotiwa kila kukicha na wahalifu wenye taaluma ya teknolojia ya mawasiliano (ICT), huiba fedha katika mashine za kutolea fedha (ATM) au katika benki kwa kutumia teknolojia hiyo.V.S
Kwa kutumia njia hii, wahalifu wana uwezo wa kujificha zaidi kuliko zama za matumizi ya kuvamia benki kwa silaha.
Kwa mara ya kwanza, Machi 2010, Sh300 bilioni ziliibwa kwa njia ya mtandao kupitia mashine za ATM.
Mshauri Mkurugenzi wa mifumo ya malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Kennedy Komba anasema benki kuu imekwishatoa mwongozo
kuhusu uhalifu wa mitandao katika mabenki.
Anasema kwa kuwa BoT inafanya kazi kwa niaba ya Serikali na mabenki, imetoa mwongozo huo kuhakikisha kuwa zinajidhatiti katika kupambana na uhalifu wa kimtandao.
"Kwa kawaida sisi tunatoa miongozo kuhusu uhalifu huo na tunatoa elimu ambayo kila mmoja anaweza kuitumia ili kujilinda na uhalifu huo," anasema
Anasema BoT imeandaa miswada mitatu ya sheria za uhalifu wa mitandao ambayo inatarajiwa kupelekwa bungeni mwakani.
"Sheria hiyo ikipita basi tutakuwa na sheria tatu mpya ambazo zitakuwa zikilenga kupambana na uhalifu huo au kwa lugha ya kitaalamu 'cybercrime'," anasema
Anasema bado kuna changamoto kubwa katika kumaliza kabisa tatizo la uhalifu wa mitandao lakini sheria pekee ndizo zinazotumika kupambana na uhalifu huo.
CHANZO:MWANANCHI
Comments
Post a Comment