DAVIDO AZIDI KUWACHEFUA WATANZANIA BAADA YA KUPOST PICHA INAYOONYESHA TAYO KUPEWA PESA NA BILIONEA WA NIGERIA $ 350,000 ZAIDI YA IDRIS

Mara baada ya fainali za Big Brother Africa Hotshot kumalizika Jumapili iliyopita, Mwanamuziki Davido wa Nigeria kutweet kwamba "They cheated again LOL" sentensi hii ilizua mjadala mkubwa mpaka kupelekea account ya Davido kujaa matusi kutoka kwa watanzania na mashabiki wengine wa Idris waliokuwa wanafatilia kwa ukaribu zaidi shindano hilo.

Mtandao wa Bongo 5 jana walipost habari ambayo ilienda kiundani zaidi na kujadili kauli hiyo aliyoiandika Davido uenda haikulenga moja kwa moja juu ya Mshiriki kutoka Tanzania kushinda kitita hicho bali alilenga zaidi maamuzi yaliyofanywa na Big.

Davido amezua lingine leo baada ya kupost picha hiyo ikionyesha jeuri iliyofanywa na Billionea wa kinigeria kutoa mkwanja ambao umezidi zawadi ya Big Brother Africa Hotshots 2014 ambapo Idris amepata $ 300,000. Account ya Davido ya Instagram imejaa zaidi ya comment elfu 3 nyingi zikimkosoa Davido na matusi juu, sijui sasa tunaelekea wapi maana mtandao wa instagram umejaa matusi yasiyokuwa na msingi wowote.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA