PICHA:MAHABUSU AFARIKI AKIJARIBU KUTOROKA KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU

JESHI la Magereza limefanikiwa kumdhibiti Mahabusu  wa Kesi ya dawa za kulevya ambaye ni Raia wa Sieralioni,  Abdul Koroma (33) asitoroke chini ya Ulinzi wa Askari Magereza ndani  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa kumtwanga risasi na kumuua papo hapo!

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, baadhi ya wanausalama waliopangwa kulinda usalama Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa kuwa wao siyo wasemaji,  walisema mtuhumiwa alikuwa anashitakiwa kwa makosa ya kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 1,229, zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 61. Kesi yake ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema.

Walisema asubuhi marehemu huyo, ambaye ni mahabusu, aliletwa mahakamani na askari magereza akiwa na mahabusu wenzake na kisha kufikishwa katika mahabusu ya mahakama hiyo, baadae mtuhumiwa aliomba apelekwe chooni kujisadia, lakini ghafla akaanza jaribio la kuparamia ukuta ili akimbie ndiyo askari waliokuwa akimsikindikiza chooni wakafyatua risasi hewani ili kumtaka aache jaribio lake, lakini inadaiwa Koroma aliendelea na jaribio lake.

"Ndipo ikabidi mmoja wa askari magereza 'ameshone risasi' yaani amefyatulie risasi Koroma ambayo ilimpata kichwani na kumsababishia mauti papo hapo! Baada ya Koroma kupekuliwa na wanausalama walikuta ndani ya soksi aliyovaa kuna kikaratasi kilichochorwa ramani na namba za simu za watu wa kumpokea hapa Dar es Salaam," kilisema chanzo changu.

Tayari mwili wa Koroma, ambaye alikuwa na kesi na P121/2013, umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.









Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA