KAMANDA WA UJERUMANI AJIVUNIA USALAMA BAHARI YA HINDI

DSC_0001
Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kwenye hafla maalum ya kuwakaribisha na kuwapongeza wanajeshi wa kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta chini ya kamanda Peter Christian Semrau (kulia) iliyofanyika ndani ya meli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
KAMANDA wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta, Peter Christian Semrau, amesema jumuiya ya kimataifa imepata mafanikio makubwa kwa kuwezesha njia inayotumika sana na meli kuwa salama.
Akizungumza katika mahojiano ndani ya meli hiyo ambayo imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, Kamanda Semrau alisema kwamba kwa mwaka huu hapakuwepo na tukio kubwa ambalo limetikisa eneo hilo la Pwani ya Pembe ya Afrika inayopakana na Somalia na Yemen.
Alisema kuanzia shughuli za kimataifa kukabili uharamia na ujambazi baharini kuanza mwaka 2009 kumekuwepo na ushindi wa kimataifa kutokana na kuendelea kupungua kwa matukio katika eneo hilo ambapo awali ilikuwa ni tishio kubwa.
Alisema pamoja na kupungua kwa matukio ya kijambazi na utekaji nyara kazi ambayo inatarajiwa kufanywa mwakani ni kuhakikisha kwamba mataifa yanayopakana na bahari ya Hindi yanawezeshwa kujilinda yenyewe dhidi ya matukio ya baharini.
Pichani juu na chini baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania na mabalozi mbalimbali waliojumuika kwenye hafla hiyo wakisiliza risala ya Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke (hayupo pichani).
Meli hiyo ambayo inafanya doria kuanzia kaskazini mwa Afrika hadi Kusini imetia nanga Dar es salaam ikitokea Madagascar ambako nako ilipata mapokezi makubwa. Operesheni Atalanta inaendeshwa na vikosi vya Umoja wa Ulaya vikilinda eneo la bahari ambalo lina shughuli nzito kwa meli za biashara.
CHANZO:JIACHIE

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA