JE WAJUA MADHARA YA KUTUMIA CHUMVI NYINGI KATIKA MATUMIZI YA CHAKULA?

Moja ya vitu ambavyo vimekuwa muhimu kwenye chakula cha mwanadamu ni chumvi
ambayo hutumika kuongeza ladha ya chakula ambacho hutumika mezani .

Umuhimu wa kiungo hiki umefikia hatua ya waswahili kuibatiza chumvi jina la utani ambalo ni Mkuu
Wa Jiko .

Hata hivyo chumvi inaweza kuwa na madhara pale ambapo inatumika kuliko kawaida na
madhara hayo ni kwa afya ya mtumiaji . Je chumvi ni mbaya kwa Afya yako? Mwili wa mwanadamu unahitaji chumvi kwa
kiwango Fulani kwani inasaidia kuongeza mnadini ambayo mwili wako unayahitaji . Hatari
ni pale unapokula chumvi nyingi kuliko kiwango ambacho mwili wako unahitaji . Imagundulika
kuwa chumvi husababisha matatizo ya shinikizo la damu hali ambayo inaweza ikaongeza uwezekano wa mtu kupata matatizo ya shambulio la moyo pamoja na hatari nyingine za magonjwa ya moyo .

Madaktari wanashauri
utumiaji wa chumvi kwa kiwango cha chini ili kuepukana na matatizo haya . Je kiasi gani cha chumvi kinazidi kiwango cha
kawaida . Kimsingi hupaswi kula zaidi ya gramu tano za
chumvi kwa siku , hii ni sawa na kijiko kimoja cha chai ambacho kina ujazo wa milligram 5 . Kiwango hiki kinajumuisha chumvi ambayo
unaongeza ukiwa unapika jikoni , chumvi unayoongeza mezani wakati wa kula na ile chumvi ambayo inapatikana kwneye chakula
kiasili hii ni kwa sababu kuna vyakula ambavyo ndani yake kuna chumvi hata kama havina ladha
ya chumvi . Mfano wa vyakula ambavyo tayari vina chumvi ndani yake ni Mikate , Sausage na
nyama za kusaga , supu ya kutengenezwa kiwandani , vyakula vya nafaka ambavyo hutumika kwenye kifungua kinywa (breakfast) na hata baadhi ya biskuti .

Je tunatumia chumvi nyingi kuliko kawaida ? Waafrika wengi huwa na kasumba ya utumiaji wa chumvi kwa kiwango kikubwa kuliko kawaidana hii imezoeleka sana kuanzia majumbani
mpaka mahotelini .

Ni rahisi sana kutumia chumvi nyingi kuliko kawaida wakati wa milo ya kila siku . Nusu ya chumvi ambayo hutumiwa na watu ni
chumvi inayopatikana kwenye vyakula hasa vile vya kutengenezwa viwandani ambayo huwekwa
wakati wa utengenezaji wa vyakula hivi huko huko viwandani ili kuvifanya vikae kwa muda
mrefu .

Nusu nyingine ni ile ambayo ambayo huongezwa jikoni na ile ambayo watu huongeza
mezani wakati wa kula ili kukoleza ladha ya chakula husika .
Nini kinatengeneza chumvi
Chumvi inatengenezwa na vitu viwili ambavyo ni sodium na chloride , Sodium ni sehemu ya
chumvi ambayo ambayo huongeza presha ya damu au kwa lugha inayoeleweka zaidi huongeza shinikizo au msukumo wa damu hasa pale unapotumia chumvi nyingi kuliko kiwango
cha kawaida . Pamoja na ukweli kwamba tunatumia chumvi nyumbani , taarifa zinaoandikwa kwenye vihifadhi vya vyakula hasa
vile ambavyo vinatengenezwa viwandani huonyesha kiwango cha madini ya sodium ambayo yametumika kwenye chumvi . Kijiko
kimoja cha chai mara nyingi huwa kina miligramu 2000 za sodium .
Ni jinsi gani tunaweza kutumia kiwango cha chini cha chumvi kwenye vyakula ?
Haiwezekani kupunguza kiwango cha chumvi ndani ya siku moja au ghafla , mabadiliko yanapaswa kufanyika hatua moja baada ya
nyingine .

Muhimu ni kujizoesha hisia ya kudhani kuwa chakula kina ladha hata pale ambapo chumvi
haijakolea Kama una kawaida ya kuongeza chumvi nyingi
mezani hatua ya kwanza ni kuondoa kile kikopo kidogo cha chumvi mezani hasa wakati wa
chakula , hii ni kwa sababu unapaswa

kukumbuka kuwa kama ulishaongeza chumvi
tangu jikoni hauna sababu ya kuongeza nyingine mezani .
Jaribu pia kupunguza kiwango cha chumvi unachoongeza wakati wa mapishi yako , unapaswa kuonja wakati ukiwa unapika ili kuepuka kuongeza kiwango cha chumvi
ambcho kinaweza kuwa hatari kwa Afya yako .

Kama chakula chako kina viungo ambavyo ndani yake kuna chumvi ya asili hupaswi kuongeza
chumvi nyingine juu yake . Katika tafiti zilizofanyika hivi karibuni
imefahamika kuwa kuna baadhi ya vitu vinavyoweza kutumika kama chuimvi ambavyo havina madhara sawa na ya chumvi kwenye mwili wa mwanadamu na mojawapo ni limao pamoja na ndimu .

Kiungo kingine kinachoweza kuchukua nafasi ya chumvi kwenye chakula chako ni mdalasini .Vyakula visivyo na chumvi nyingi?
Vyakula ambavyo havijatengenezwa kiwandani kwa maana ya vyakula halisi mara nyingi huwa havina chumvi nyingi na hii inamaanisha kuwa unapaswa kuchagua vyakula vya asili kuliko vile ambavyo vimetengenezwa viwandani .

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA