DAKTARI FEKI ANASWA MUHIMBILI KATIKA TAASISI YA MOI

Moja kati ya matukio yaliyochukua headline ni hili tukio la kukamatwa Daktari feki,Dismas Macha katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) akiwa amevaa sare za kazi kama Daktari ambapo hii inakuwa mara ya pili kukamatwa akiwa anachangisha rambirambi kwa Madaktari akidai kuwa amefiwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo ya MOI, Dk Othman Wanin Kiloloma amesema; “Tumekuwa tuna tatizo kubwa la kuletewa watu wanaokuja wao na kujitia ni madaktari wakiomba watu pesa, wakiomba waweze kupewa takrima na hata michango mingine na wamefikia hatua sasa ya kuwatapeli hata madaktari wenyewe kwa kuomba michango na vitu vingine
Leo tumewaita Waandishi wa Habari kuwaeleza kisa cha mtu ambee amekuja na kujitia yeye ni Daktari wa sehemu ya taasisi na anaomba michango mbalimbali, na mtu huyu sii mara ya kwanza amekuwa akishikwa Muhimbili sehemu tofauti kwa wakati tofauti kwa hiyo tumewaita ili muweze kumtambulisha kwa jamii asiweze kudanganya watu wengine kwamba yeye ni Daktari”– Dk. Kiloloma.
Mwananchi mmoja ambaye alikuwa mmoja ya watu walishuhudia mtu huyo kukamatwa amesema; “Suala la Madaktari feki tatizo kubwa lililopo sio Madaktari feki kama hivyo kuna Mahakimu feki, Madaktari feki, ukishaona mahali popote anatokea mtu feki ujue kuna maslahi na tatizo kubwa linalojitokeza kwenye Hospitali ni ukifika Madaktari wenyewe halisi wanataka fedha ili wakuhudumie, kwa hiyo yoyote anaweza kujifanya feki kwa maana anakusanya fedha za Watanzania alafu anatoweka kwa hiyo anakuwa amekula fedha…

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA