DIAMOND PLATNUMZ KUFANYA SHOW YA BURE NCHINI UJERUMANI KUWAPOZA MACHUNGU MASHABIKI WAKE.

Diamond Platnumz pamoja na management yake  waamua kufanya show ya  BUREEEE nchini Ujerumani baada ya zile fujo zilizotokea nchini humo, zilizotokana na kuchelewa kufika ukumbini badala ya saa 4  usiku akafika kwenye show saa 11 alfajiri.

Show hiyo itafanyika tarehe 20 September katika mji ule ule wa Stuttgart ili kuwapoza machungu ya vurugu zote zilizotokea na kurudisha heshima ya jina lake vizuri lililoharibika kutokana na vurugu hizo.

Kupitia account yake ya instagram mkali wa "mdogo mdogo" ameandika maneno haya.

"YES!!!! STUTTGART GERMANY!!! on this 20th of September 2014... kiukweli nilisikitishwa sana na kilichotokea last time Stuttgart... lakini baada ya kugundua kuwa pia lilikuwa ni kosa la mtu mwingine na si promotter kama nilivyodhani, yaani Brittis Events... ndipo tulipoamua na kuwaletea Burudani hii Mashabiki zetu pendwa wa Stuttgart....hakikisha ufikapo unapendeza zaidi maana kama ujuavyo safari hii Vyombo vyote vya habari ndani na nje ya nchi vitakuwa pale kwa RedCarpet.... kiingilio ni BUREEEEEE!!!... tafadhariwambie na wenzio wa nchi za karibu...#NORWAY #HOLLAND #SWITZLAND #BELGIUM #SWEEDEN na kadharika"

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA