TAKRIBANI WAUMINI 44 WA SINAGOGI LA T.B JOSHUA WAPOTEZA MAISHA

Sehemu ya jengo lililoanguka. (picha: blogu ya Miss Petite Nigeria)


Shirika la habari la kimataifa la
CNN limechapisha habari kuwa inakadiriwa watu 44 wamepoteza uhai baada ya nyumba ya kufikia wageni iliyomo ndani ya Kanisa kubwa la mhubiri maarufu, T.B. Joshua lijulikanalo kwa kimombo, "The Synagogue, Church Of All Nations" (Sinagogi, Kanisa la Mataifa Yote) lililopo Lagos nchini NIgeria, lilipoanguka mchana wa siku ya Ijumaa iliyopita.

CNN inanukuu afisa wa wakala wa uokozi, Ibrahim Farinloye, ambaye ni msemaji wa National Emergency Management Agency, kuwa alitoa taarifa hiyo jana Jumapili na kwamba watu wapatao 130 waliokolewa kutoka kwenye kifusi na huenda wapo zaidi wanaohitaji kunasuliwa.


Jengo hilo lilianguka wakati ujenzi wa kupanua na kuongeza ghorofa tatu ukiendelea.


Inaelezwa kuwa shughuli za uokozi zilichelewa kwa kuwa baadhi ya waumini waliwakatalia

waokoaji kuingia ndani.

Baadhi ya maripota waliokuwa wakirekodi ajali hiyo walishambuliwa na baadhi ya waumini wenye hasira ambao walipora vitendea kazi vyao kama vile kamera ili kuzuia wasirekodi jengo hilo lkianguka.


T.B. Joshua mwenyewe alipohojiwa kuhusiana na ajali hiyo, aliomba radhi kwa walichokifanya waumini wake kwa waokozi na waliokuwa wakirekodi tukio hilo, na kulliambia gazeti moja hapo jana Jumapili kuwa ndege iliyopaa na kuzunguka jengo hilo mara kadhaa, huenda ikawa ndiyo sababu ya kuanguka kwa jengo hilo.

“Immediately I left the prayer room (which is a 10-minute drive form the church) for the church, I got a call that a jet was hovering over the prayer room but as I finished bathing and moved to the prayer room, I got another call that the jet has moved to the church and that was it,“Members cannot be the target, the easier way to stop this church is to get the head and from my explanation, you know the truth.” (imenukuliwa)
Lakini, shirika la habari la NEMA katika ukurasa wake wa Facebook linatoa taarifa tofauti likisema huenda ghorofa mbili zilizoongezwa bila ya kuweka kwanza msingi imara, ndicho chanzo cha kuanguka kwa jengo hilo.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA