Polisi Uganda wamewakamata washukiwa 19 wa Alshabab
Polisi nchini Uganda wanasema kuwa wamekamata
kiasi kikubwa cha vilipuzi walipokuwa wakifanya operesheni ya kutibua
jaribio la shambulizi la kigaidi la wanamgambo wa al-Shabab.
Hadi
sasa, watu kumi na tisa wamekamatwa na polisi na wanahojiwa kuhusiana na
nia yao kutekeleza vitendo vya kigaidi, kulingana na msemaji wa polisi.
Wiki
iliyopita, ubalozi ya Marekani mjini Kampala ulionya kuwa kulikuwa na
uwezekano wa shambulizi la kulipiza kisasi mauaji wa kiongozi wa kundi
hilo la Al-Shabab.
Uganda inalaumiwa kwa kutuma majeshi yake kupigana chini ya Umoja wa Afrika Amisom.
Marekani ilitangaza kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Alshabab Ahmed Abdi Godane baada ya shambulizi la angani Septemba 2 .
Serikali inasema kuwa kundi hilo la kigaidi lilikuwa limepanga kushambuliz mji mkuu wa Kampala.
Askari walisema kuwa kundi hilo lilikuwa limepanga kufanya mashambulizi katika miji mingine mwishoni mwa wiki.
Siku ya Jumapili, Marekani ilifuta onyo lao ikidai kuwa iliamini kuwa tishio la shambulizi lilikuwa halipo tena.
Waziri
wa habari nchini Uganda, Rose Namayanja aliwasihi wananchi kuendelea
kuwa waangalifu huku serikali ikiendelea kufanya uchunguzi wa
mashambulizi yoyote yaliyokuwa yamepangwa.
Alisema kuwa watuhumiwa walikuwa wamepatikana na vifaa vinavyotumiwa katika vitendo vya kigaidi na nia yao ilikuwa wazi sana.
chanzo:bbc swahili.
Comments
Post a Comment