Posts

Showing posts from December, 2014

NAWATAKIA MWAKA MPYA MWEMA NA WENYE MAFANIKIO TELE.

Image

AIRASIA QZ8501: MIILI YAANZA KUWASIL INDONESIA

Image
Wanajeshi wakiwa wamebeba miili ya mwanzo ya watu waliokufa katika Ndege ya AirAsia. MIILI ya mwanzo ya watu wawili waliokuwa kwenye Ndege ya AirAsia QZ8501 imewasili leo jijini Surabaya, Indonesia ambapo ndugu na jamaa wanasubiri kwa utambuzi. Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200, ilipotea Jumapili iliyopita ikiwa imebeba watu 162 ikitokea Surabaya kwenda Singapore, ambapo baadhi ya miili imeanza kupatikana jana katika Bahari ya Java. Watu 155 kati ya 162 waliokuwa katika ndege hiyo ni  raia wa Indonesia.

SAMANTHA APOKELEWA KWA MIKONO MIWILI KATIKA FAMILIA YA IDRIS WA BIG BROTHER

Image
Mapenzi urafiki wa Idris Sultan na mrembo wa Afrika Kusini aliyekuwa swahiba wake wa karibu kwenye shindano la Big Brother Africa, Samantha, umefika kwenye hatua ya juu zaidi. Samantha ambaye bado yupo nchini amepokelewa kwa mikono miwili na familia ya Idris.   “They’ve only been good to me and I can’t say thank you enough. How people can love you this much but only no you a few weeks is beyond me,” ameandika Samantha kwenye picha akiwa na familia ya Idris. “God bless your beautiful hearts . Thank you ! Thank you ! Thank you.” Katika picha nyingine akiwa na Idris, mrembo huyo ameandika: And there was light . When you trying to take a selfie and someone else is taking a pic of you.#Lastnight#selfielife#baemuch#thisnigga#love#peace#happiness#godfirst.”   Wakati huo huo Samantha ametumika kama mrembo kwenye kava la wimbo wa Millian, Until Forever Ends.

TIZAMA KILICHOMTOKEA MWIZI HUYU ALIPOTAKA KUIBA PESA KWENYE ATM

Image
Siku za mwizi ni arobaini, huyu zake zilifika hivi. Jamaa mmoja  Australia  alifika katika  ATM  lengo lake likiwa ni kuiba, akategesha kitu ambacho ni kama baruti hivi ili mashine ilipuke aibe pesa. Mpango wake ulikwama, ulitokea mlipuko mkubwa kwenye  ATM  ambao ulimtupa mbali, akainuka na kukimbia huku mashine ya  ATM  ikiwa imeharibika vibaya kutokana na mlipuko huo. Polisi wa Jiji la  Darwin ,  Australia  ilikotokea tukio hilo wanahisi jamaa huyu anahusika na tukio la namna hiyo ambalo lililotokea siku ya Sikukuu ya Christmas.  itazame hapa video ya tukio zima

BINTI AJIRUSHA BAHARINI

Mwanadada mmoja amejirusha baharini katika kivuko cha ferry mapema leo adhuhuri wakati akiwa ameabiri ferry ya MV Harambee kutoka upande wa Mombasa Kisiwani kuelekea Likoni. Msichana huyo mwenye umri kati ya miaka 20 na 25 amejirusha kutoka eneo la juu ya ferry wakati fery ikiwa katikakati ya bahari ikielekea ufuoni. Wapiga mbizi wa shirika la Kenya ferry wamejaribu kuokoa maisha yake baada maji kumzidi kutokana na mawimbi makali na akafanyiwa huduma ya kwanza na hatimaye kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Likoni. Kwa sasa anapokea matibabu katika hospitali moja mjini Mombasa. Kulingana na afisa wa uhusiano mwema wa shirika la Kenya Ferry Harun Mutiso amesema kwamba maafisa wa polisi wanachunguza kilichopelekea msichana huyo kutaka kutoa uhai wake. Hata hivyo kulingana na walioshuhudia ni kwamba wanadada huyo alionekana mtulivu na hakuna aliyetarajia kwamba anaweza jirusha kutoka eneo la juu ya Ferry hadi ndani ya bahari. Haya yanajiri siku moja baada ya mwanadada mmoja kutoka mtaa

PICHA:MAHABUSU AFARIKI AKIJARIBU KUTOROKA KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU

Image
JESHI la Magereza limefanikiwa kumdhibiti Mahabusu  wa Kesi ya dawa za kulevya ambaye ni Raia wa Sieralioni,  Abdul Koroma (33) asitoroke chini ya Ulinzi wa Askari Magereza ndani  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa kumtwanga risasi na kumuua papo hapo! Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, baadhi ya wanausalama waliopangwa kulinda usalama Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa kuwa wao siyo wasemaji,  walisema mtuhumiwa alikuwa anashitakiwa kwa makosa ya kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 1,229, zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 61. Kesi yake ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema. Walisema asubuhi marehemu huyo, ambaye ni mahabusu, aliletwa mahakamani na askari magereza akiwa na mahabusu wenzake na kisha kufikishwa katika mahabusu ya mahakama hiyo, baadae mtuhumiwa aliomba apelekwe chooni kujisadia, lakini ghafla akaanza jaribio la kuparamia ukuta ili akimbie ndiyo askari wa

MAGAZETI YA LEO JUMANNE

Image

JE WAJUA MADHARA YA KUTUMIA CHUMVI NYINGI KATIKA MATUMIZI YA CHAKULA?

Image
Moja ya vitu ambavyo vimekuwa muhimu kwenye chakula cha mwanadamu ni chumvi ambayo hutumika kuongeza ladha ya chakula ambacho hutumika mezani . Umuhimu wa kiungo hiki umefikia hatua ya waswahili kuibatiza chumvi jina la utani ambalo ni Mkuu Wa Jiko . Hata hivyo chumvi inaweza kuwa na madhara pale ambapo inatumika kuliko kawaida na madhara hayo ni kwa afya ya mtumiaji . Je chumvi ni mbaya kwa Afya yako? Mwili wa mwanadamu unahitaji chumvi kwa kiwango Fulani kwani inasaidia kuongeza mnadini ambayo mwili wako unayahitaji . Hatari ni pale unapokula chumvi nyingi kuliko kiwango ambacho mwili wako unahitaji . Imagundulika kuwa chumvi husababisha matatizo ya shinikizo la damu hali ambayo inaweza ikaongeza uwezekano wa mtu kupata matatizo ya shambulio la moyo pamoja na hatari nyingine za magonjwa ya moyo . Madaktari wanashauri utumiaji wa chumvi kwa kiwango cha chini ili kuepukana na matatizo haya . Je kiasi gani cha chumvi kinazidi kiwango cha kawaida . Kimsingi hupaswi kula zaidi

KOCHA PATRICK PHIRI KIBARUA CHA KUINOA SIMBA CHAFIKIA KIKOMO

Image
Ni kama episode sasa iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu, mara baada ya Yanga kumtimua kocha wake Maximo baada ya mechi ya mtani Jembe sasa ni kwa upande wa Simba Sports club nao wanachukua headline nyingine ya kumfukuza aliyekuwa kocha wake mkuu kutoka Zambia Patrick Phiri na bechi lake lote la ufundi wametimliwa. Leo atapewa barua na haki zake za msingi zitafuatwa kabla ya kuondoka,nafasi yake itachukuliwa na kocha MSERBIA GORAN ambaye alishawahi kuifundisha POLICE ya RWANDA ndiye rasmi kocha wa Simba na atasain mkataba siku ya j5 jioni. Mserbia huyo atasaidiwa na kocha kutoka Rwanda anaitwa JEAN MARIE NTAGAWABILA. Hiyo ndiyo habari ya mtaa wa msimbazi

BASI LA OSAKA LAPATA AJALI MKOANI MARA

Image
Basi la osaka lenye namba za usajili  T 202 CVS linalofanya safari zake kutoka Musoma- Dar lapata ajali wilayani Bunda mkoani Mara  asubuhi hii. Mtoa taarifa hakuna aliyefariki katika basi ilo lakini kuna majeruhi kadhaa. Mtoa taarifa anasema aliyesababisha ajali ni mwendesha baskeli

NYALANDU AJITOSA RASMI MBIO ZA URAIS KUPITIA CCM 2015

Image
WAZIRI wa maliasili na utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini(CCM) ,Lazaro Samwel Nyalandu, ambaye ametangaza rasmi kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.   Na Gasper Andrew, Mwananchi   WAZIRI wa maliasili na utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini(CCM) ,Lazaro Samwel Nyalandu,ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani. Nyalandu ametangaza nia hiyo leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ilongero Jimbo la Singida kaskazini. Alisema baada ya kutafakari kwa muda mrefu na kujikagua kwa kina,ameona anao uwezo wa kutosha wa kuweza kupokea kijiti kutoka kwa rais anayemaliza muda wake mwakani kwa mujibu wa katiba. “Kujikagua huko ni pamoja na kutafakari jinsi alivyoweza kutekeleza ilani ya uchaguzi ya

MAONI YA MDAU KUHUSU HOTUBA YA RAIS ALIPOZUNGUMZIA ESCROW

Wengi tumemshangaa Rais wetu kwa jinsi alivyokuwa amejiekeza kuwatetea wahalifu na kamwe hakuonyesha uchungu wa hasara iliyosababishwa na wezi wale! Katika nchi wanakotoka hao vibaka kosa la kukwepa kodi lingewagharimu hata mali na kampuni kufilisiwa; lakini la kustaabisha hapa ni Mkuu wa nchi mwenyewe alipanda ulingoni kuwatetea kana kwamba naye ni mmiliki mmojawapo wa hisa katika IPTL! Jingine lililotuacha midomo wazi ni eti na yeye kufanya uchunguzi ndani ya uchunguzi! CAG alishafanya uchunguzi, Kamati ya Bunge walifanya uchunguzi uliopitiwa, kukosolewa na kusahihishwa ilipobidi na Bunge zima; na vyote hivyo ni vyombo vya serikali hii hii; watu wanajiuliza; haviamini vyombo vilivyoaminiwa na kupewa dhamana hivi au anataka kuleta FBI?  Tungemwelewa endapo angetwambia waliopokea fedha na aliyegawa wangekatwa, kuhojiwa na kuchunguzwa; lakini hili la kurudia uchunguzi uliokwishafanywa kwa lengo la kuwatoa hatiani watu waliothibitika kukosea ni la kushangaza n

FUMANIZI LA X-MASS UMELIONA? PITA HAPA

Image
Stori: Deogratius Mongela na Chande Abdallah Shabaash! Mwanamke mmoja, mkazi wa Mikocheni A, Dar, Catherine Kayombo ‘Catty’ anadai kumfumania mumewe aliyemtaja kwa jina la Excavery Kayombo akiwa na mchepuko alioutaja kwa jina la Mariamu Kauke ‘Mamuu’ ndani ya Sikukuu ya Krismasi ‘X-Mas’, Ijumaa Wikienda limesheheni. Mchepuko unaojulikana kama Mariamu Kauke ‘Mamuu’ ukiwa katika kitanda cha mume wa mtu. MAJIRANI WAPENYEZA UBUYU Tukio hilo la aina yake lilitokea majira ya mchana maeneo ya Mikocheni A ambapo Catty anayedai kupigwa na mumewe na kwenda kwao, alipata taarifa (ubuyu) kutoka kwa majirani kuwa mumewe ameingiza mwanamke nyumbani kwake na wanajiachia na kujimwayamwaya kila mahali ndani kama kumbikumbi. Mchepuko ukikemea kupigwa picha dirishani. Baada ya kupata taarifa hizo, Catty alikwenda nyumbani kwake kisha akamfuatilia mumewe na mwanamke huyo hatua kwa hatua kupitia dirisha la chumba chao ‘kwa baba na mama’. Mume wa mtu, Excavery Kayombo akiwa na mch

DUDE: MWAKA 2014 NI GUNDU KWANGU

Image
Stori: Gladness Mallya TUKIWA tunaelekea ukingoni mwa mwaka, msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa mwaka 2014 ulikuwa hauna bahati (gundu) hivyo anamuomba Mungu huo ujao uwe wa baraka kwake. Msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’. Akipiga stori na gazeti hili, Dude alisema ndani ya mwaka huu hakuweza kufanikisha lengo lolote kati ya yale aliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa jambo ambalo linamuumiza kwani alitegemea kufanya mambo mengi lakini hakufanikisha. “Nilitegemea kufunga ndoa lakini imeshindikana kwa sababu upande wa kazi mambo hayakuwa mazuri pia nilipanga kwamba kipindi changu cha Bongo Dar es Salaam kitarudi hewani lakini ikashindikana, ukweli mwaka huu haukuwa mzuri kabisa kwangu namuomba Mungu ujao akanifanikishe malengo yangu,” alisema Dude.

UNAIJUA AINA YA WATU WANAONYONYA NGUVU ZA WENGINE?

Image
Shukurani kwa Imani Ngwangwalu kwa kutushirikisha makala iliyopachikwa hapo chini. Mawasiliano yake yamepachikwa hapo mwishoni. Inaweza kuonekana kama ni kitu cha kushangaza lakini huu ndio ukweli wapo watu wanaonyonya nguvu za watu. Watu hawa wana uwezo wa kumwandama mtu hadi anakufa bila kujua. Watu hawa hawajafa,wako hai na tunaishi nao, wengine wakiwa ni watu wetu wa karibu sana, kama wazazi, wapenzi, watoto, jirani, marafiki au mabosi wetu. Hufanya vipi kunyonya nguvu zetu? Hutumia njia za aina mbalimbali, ambazo huzaa matunda kweli. Mtu anaweza kuuliza, inawezekana vipi mwingine anyonye nguvu zangu na hizo nguvu ni zipi? Kwa mfano, mimi ninapo kuwa nakukera kila siku, ninakugusa kihisia. Ninapokugusa kihisia, unaumia kihisia na kimwili. Baada ya muda Fulani wa kero zangu, nakuwa nimekupa athari kubwa kimwili na kiakili bila mwenyewe kujua na kama imeshawahi kukutokea umekerwa na mtu huwa inapelekea hata unapokutana na mtu huyu anayekukera

USIKU WA USWAZI NA WASWAZI NI NOMAAA DAR LIVE

Image
Msanii Inspector Haroun akiimba na mashabiki wake. Chid Benz kavua shati baada ya mzuka kumpanda.… Msanii Inspector Haroun akiimba na mashabiki wake. Chid Benz kavua shati baada ya mzuka kumpanda. Mesen Selekta akiimba kanyaboya pamoja na wacheza shoo. MC na Muimbaji, Pam D akizungusha nyonga. Mnyama, TID akiwa na kimwana stejini. Kundi la Umeme wakifanya yao stejini. Kala Pina akikumbushia ngoma za kitambo. Wabibi wakikamua. Kundi la Yakuza Mobb wakikamua. Wadau wa muziki wakiwa stejini. JANA katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar, wasanii kibao wamedondosha bonge la shoo katika Usiku wa Uswazi na Waswazi, shoo iliyoandaliwa na Defatality Music ikiwashirikisha mastaa wakongwe kama Chid Benz, Top in Dar ‘TID’ ,Yakuza Mobb, Kalapina, aka “Mbuge Mtarajiwa’’, Pam D pamoja na wasanii kibao wanaokuja kwa kasi wakiwemo Kundi la Umeme na Wabibi. Wasanii wengine waliodondosha