Raia wa Nigeria akamatwa JNIA na kete 100 za cocaine

19 Mar20
RAIA wa Nigeria, Anthony Ifeanyichukwa Okafor (52), amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akidaiwa kumeza kete 100 za dawa za kulevya aina ya cocaine ambazo thamani yake bado haijafahamika.

Tukio hilo limetokea takribani siku 22 baada ya raia mwingine wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) kuvunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika uwanja huo.

Cole alikamatwa Jumatatu ya Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo. 
 
Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alisema jana kuwa amefika nchini kumfuata rafiki yake wa kike aliyekutana naye Hong Kong, China na baadaye Douala, Cameroon.

Nzowa alisema mtuhumiwa huyo alisema rafiki yake huyo wa Tanzania ni mpenzi wake na wako pamoja katika kazi hiyo.

Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani alisema wauzaji wa dawa hizo siku hizi wamegundua mtindo mpya wa kuwatumia watu wazima ili wasigundulike kutokana na mwonekano wao.

  • Taarifa kwa mujibu wa blogu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA