Taarifa ya ajali nyingine ya basi leo Morogoro

IMG-20150319-WA0040

Watu 7 wamefariki na wengine 26 kujeruhiwa baada ya basi la Msanga Expresslililokuwa linatokea Morogoro kwenda Mahenge kugongana na basi la Luwinzolililotokea Njombe kwenda Dar katika eneo la mbuga ya Mikumi.
DSC_0351
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi ambapo dereva wa basi la Msanga alikuwa akijaribu kulipita lori, basi hilo likagongwa upande wa kulia na kusababisha vifo vya watu sita hapo hapo na mwingine mmoja kufariki  wakati akiwa anakimbizwa kupelekwa Hospitali.
DSC_0352
Kamanda wa Polisi  Morogoro, Leonard Paulo amesema mwili mmoja ndio uliotambulika na miili mingine 6 imehifadhiwa katika Hospitali ya St. Kizito Mikumi, madereva wa mabasi yote wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu chini ya ulinzi.
Ilipofika hapa mvua ilikuwa inavyesha na kulikuwa na utelezi.. kilichotokea ni kwamba mbele kulikuwa na lori ambalo limetoroka kwenye eneo la tukio, kwa hiyo baada ya kuliona lori alitaka kulipita kwa upande wa  kulia wakati analipita huyo mwenye basi kwa mbele ghafla kulikuwa na gari lingine”– Kamanda wa Polisi  Morogoro, Leonard Paul.
DSC_0353
Muunguzi wa zamu Katika Hospitali ya St. Kizito, Joseph Masenga amekiri kupokea majeruhi 26 na kusema kwa sasa wanaendelea vizuri na matibabu.
DSC_0344
DSC_0345
DSC_0348
chanzo: millard ayo

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA