PICHA: MWANACHUO ALIYEJIRUSHA KUTOKA GHOROFA YA TATU AVUNJIKA MFUPA WA BEGA

 
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Cecilia Mosha (26) aliyejirusha kutoka ghorofa ya tatu hadi chini akiugulia maumivu.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Cecilia Mosha (26) aliyejirusha kutoka ghorofa ya tatu hadi chini kutokana na hofu ya moto uliotokea katika Hosteli ya Mabibo, amevunjika mfupa wa bega. Mwanafunzi huyo alijirusha kupitia dirishani juzi katika harakati za kujiokoa na moto baada ya jengo la wasichana, Block B kushika moto. " Nilisikia kelele za moto nikiwa chumbani na nipotoka nje nikakuta moshi umetanda kila kona, baada ya kuona hivyo niliona ni vema nijiokoe kwa kujirusha kutoka ghorofa ya tatu ya bweni hilo hadi chini kupitia dirishani,” amesema Cecilia Mosha.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA