PICHA: MAMIA WAMZIKA ABDUL BONGE KIJIJINI KWAO MKUYUNI, MATOMBO MKOANI MOROGORO


Maziko ya Mwanzilishi na aliyewahi kuwa Meneja wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge yakifanyika leo kijijini kwao Mkuyuni, Matombo mkoani Morogoro.
Mwili wa Abdul Bonge ukiombewa kabla ya maziko leo.
Wanamuziki mbalimbali wakiwemo Shetta, Diamond Platnumz, Profesa J, Quick Racka wakishiriki maziko ya Abdul Bonge.
Mwanamuziki Diamond Platnumz akishiriki swala ya kumuombea marehemu.Mwili wa Abdul Bonge ukitolewa ndani kupelekwa eneo la kuombewa.
Mdogo wa marehemu Abdul Bonge ambaye ni Meneja wa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’ akilia wa simanzi juu ya jeneza lenye mwili wa kaka yake.
Bab Tale akiwa na majonzi baada ya mwili wa kaka yake kutolewa nje.
Waombolezaji wakijaribu kumtuliza Bab Tale.
Wanamuziki Shilole (kushoto), Madee (katikati) wakiwa na Meneja wa TMK Wanaume Family, Yamoto Band na Diamond, Said Fella wakati wa mazishi ya Abdul Bonge leo mkoani Morogoro.
Wanamuziki Dully Sykes, Diamond Platnumz na Shetta wakiwa katika mazishi ya Abdul Bonge leo.
HATIMAYE mdau wa muziki nchini ambaye ni Mwanzilishi na aliyewahi kuwa Meneja wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul  Shaban Taletale 'Abdul Bonge' amezikwa leo Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro.
Mamia ya waombolezaji wakiwemo wanamuziki Diamond Platnumz, Dully Sykes, Shetta, Shilole, Dogo Janja, Profesa J, Quick Racka na wengineo wameshiriki mazishi ya Abdul Bonge.
Abdul Bonge alifariki dunia jioni ya Machi 28 mwaka huu baada ya kuanguka alipokwenda kusuluhisha ugomvi wa rafiki yake maeneo ya Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam.
Mtandao huu unatoa pole kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Abdul Bonge kwa msiba huu uliotokea.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU ABDUL BONGE MAHALI PEMA PEPONI. AMEN.
(Picha zote na Dustan Shekidele, GPL, Morogoro)

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA