BARUA NZITO KWA BONGO MUVI: HILI LA UKIMWI MLITAZAME KWA JICHO LA TATU

Leo nimewakumbuka kupitia barua sababu wengi wenu huwa hatupati muda wa kuzungumza. Naamini kwa barua hii ujumbe utawafikia wengi kwa wakati mmoja.Dhumuni la barua hii ni kutaka kuwakumbusha kuhusu suala zima la ugonjwa wa Ukimwi (Ngoma). Hakuna asiyejua kwamba ugonjwa huu ni hatari na unaua.
Ndugu zangu, nimeguswa kuwaandikia barua hii sababu ukweli ni kwamba aina ya maisha yenu wengi wenu nayajua. Mara kwa mara tumekuwa tukisoma kuhusu nyinyi kushea mabwana na mabibi kwenye magazeti yetu.
Hiyo inaonesha ni jinsi gani mpo katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba, mastaa wengi wa kike wanaishi kwa kutegemea mabwana, hii ni hatari.
Kwa nini msifanye kazi zenu za kuigiza ambazo zimewapa umaarufu. Sanaa si ndiyo imewafanya muwe maarufu? Kwa nini mnaamua kuiweka kando?Hamtaki kufanya kazi, mnataka kugombea mabwana wenye nazo. Mbaya zaidi mabwana wenyewe mnaowagombea ndiyo walewale, fulani anamuona mwenzake anatembea na mtu fulani basi na yeye anamzunguka kwa tamaa ya fedha.

, Nasibu Abdul ‘Diamond’Hata huyo anayemzunguka mwenzake naye inafika wakati anapokonywa na mtu mwingine. Katika mzunguko huo mmoja akiwa muathirika basi wote mmekwenda na maji.

Baadaye msururu wa mabwana unahamia kwenda kwa mastaa wenzenu wa filamu, nao kila kukicha mnabadilishana. Leo utasikia fulani anatembea na fulani kesho amehamia kwa mwingine.Mastaa wa kiume wanatumia kigezo cha kudai watawachezesha sinema wasanii wachanga, ngono zembe inatawala, hakuna tena kuwapa hata hizo nafasi za kuigiza.

Jamani katika ulimwengu huu wa sasa si wa zama zile. Watu wanapaswa kubadilika, kuishi kisasa, kujitambua afya na kujikinga.Elimu imetolewa ya kutosha, hakuna mtu asiyejua. Kwa nini muendelee kufanya ngono zembe wakati mnatambua madhara yake? Kwa nini tunayahatarisha maisha yetu kiasi hiki? Tubadilike!

Mastaa wa kike badilikeni, fanyeni kazi msitegemee mabwana. Watanzania waliwajua kupitia sinema na michezo ambayo mlikuwa mkiigiza, komaeni kupitia kazi hizo za sanaa muweze kutengeneza kazi nzuri ambazo mtaziuza ndani na nje ya nchi.

Tumechoka kusikia habari za kukwapuliana mabwana. Tuseme inatosha kufanya ngono zembe.
Ni matumaini yangu mmenielewa, nawatakia kazi njema!
 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA