VIONGOZI WA DINI WAMJIA JUU KINANA

Viongozi wa dini wamjia juu Kinana
Kamati ya amani ya Madhehebu ya dini Mkoa wa Dar es Salaam imemtaka Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bw. Abdulrahman Kinana, kuwa makini na kauli anazozitoa dhidi ya viongozi na watendaji wa serikali, hususani wale wanaolalamikiwa na wananchi.Sheikh Salum ametaja moja ya kauli zilizotolewa na Kinana kuwa ni pamoja na ile aliyomtuhumu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwa amekuwa ni mtu wa kupenda kusafiri pasipo kushughulikia kero za wananchi.
Kwa mujibu wa Sheikh Salum, kauli kama hiyo ni ya kukatisha tamaa kwa viongozi wachapakazi kama waziri Nyalandu, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akionesha uzalendo kwa taifa lake kwa jinsi anavyoshughulikia tatizo la ujangili na uwindaji haramu.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA