EBOLA YATUA MAREKANI
Mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa hatari
wa virusi vya Ebola amegundulika nchini Marekani, imethibitishwa katika
mji wa Dallas, Texas.
Maafisa katika kituo cha afya cha Texas
katika hospitali ya Presbyterian wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa
ametengwa katika hospitali hiyo.
Mgonjwa huyo anasemekana kuwa ni
mtu anayeaminika kuambukizwa ugonjwa huo nchini Liberia kabla ya
kuonyesha dalili za ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 3,000 tayari
wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi na
idadi ndogo ya wafanyakazi wa Marekani wa mashirika ya misaada wamepata
nafuu baada ya kupelekwa kutibiwa Marekani.
Jumatatu, maafisa wa
kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya Dallas
wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa virusi vya
Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo.
Shirika la Afya Duniani,
WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000 wamekufa kutokana na virusi
vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka Liberia.
Nchini Nigeria,
nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kuna wagonjwa 19
waliothibitika kuugua ugonjwa wa Ebola na watu wanane wamekufa tangu
mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa nchini humo mwezi Julai.
Kuna mgonjwa mmoja aliyethibitika nchini Senegal, lakini hakuna taarifa za kifo mpaka sasa.
Ebola ni ugonjwa hatari wa virusi kuwahi kuzuka duniani.
Chanzo: bbc swahili
Comments
Post a Comment