JESHI LA POLISI ZANZIBAR LIMEPIGA MARUFUKU WAFUASI WA VYAMA KWENDA KWENYE MIKUTANO YA SIASA

Jeshi la Polisi Zanzibar limepiga marufuku kwa wafuasi wa vyama vya siasa kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine kutohudhuria mikutano ya vyama vya siasa ikiwa ni njia mojawapo ya kuepusha fujo na uharibifu wamali za umma.
Msimamo umetolewa na jeshi la polisi kupitia kwa naibu mkurugenzi namakosa yajinai DCP Salum Msangi wakati akizungumza na waandishi wa habri kuelzea maazimio yaliyofikiwa na vyama vya siasa baada ya fujo na gasia zilizotokeza wiki iliyopita ambapo wafuasi wa CUF walivamiwa na kujeruhiwa wakati wakirudi mjini kutoka makunduchi wilaya ya kusini amesema azimio hilo na mengine ikiwemo ya kufuatwa kwa sheria za usalama barabarini na kupiga marufuku matusi kwmeye mikutano hata hivyo uamauzi huo hautozuia mikutano ya wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Mkuu huyo wa upelelezi na makosa ya jinai pia alizungumzia suala la kukamtwa kwa msichana mzanzibari Ummurikhair Sadir huko mpakani mwa Kenya na Somalia kwa kuhusishwa na suala la kujiunga nakikundi cha Alshabab ambapo amesema hadi sasa hawajapatiwa taarifa yeyote na polisi wa Kenya na polisi wa kimataifa.
Hatua hiyo ya polisi kutoa maazimio hayo inatokana na fujo za hivi karibuni za harakati za kisiasa zilioanza kujitokeza ikiwemo za uchomajimoto wa maskani za CUF na kupigwa kwa wafuasi wa chama hicho wakati wakirudi mkutanoni wa hadhara.
Comments
Post a Comment