KITABU SAUTI CHA "MTEMI MIRAMBO" KUUINGIA SOKONI HIVI KARIBUNI

Mtangazaji wa zamani  wa kituo cha radio cha jijini Mwanza RFA, Fredrick Bundala kwa sasa Mhariri mkuu wa tovuti ya bongo5 ameamua kutoka kitofauti kwa kutoa kitabu sauti (Audio Book) kinachojulikana kwa jina la "Mtemi Mirambo Sultan Mkuu wa Afrika". Kitabu hiki kitakuwa kwa njia ya sauti katika CD,  kitabu sauti kitaingia sokoni hivi karibuni na kitakuwa kikipatikana kwa shilingi elfu tano (5000).

Kitabu sauti hiki sio kwa watoto tu bali kimelenga watu wote kuweza kujua historia ya mashujaa mbalimbali wa Tanganyika, kitabu sauti kinarahisisha wale wavivu wa kusoma vitabu kuweza kusikiliza kwa sauti wakati wowote ule bila kuchoka.

Unaweza kuanza kuweka order ya kitabu sauti kupitia account yake ya facebook Fredrick Bundala mfollow pia account ya instagram kwa jina la "skytanzania"




Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA