BLATTER: RAIS WA FIFA ASHANGAZWA KUMUONA MESSI AKIPEWA TUZO YA MCHEZAJI BORA

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Joseph Sepp Blatter ameungana na wadau wa soka wanaopinga hatua ya mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Andres Messi kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.
Sepp Blatter rais wa FIFA


Blatter ameustaajabisha ulimwengu kwa kuungana na kundi hilo, alipokuwa akijibu swali la muandishi wa habari kutoka nchini Hispania ambaye alitaka kufahamu ni vipi raisi huyo wa FIFA alivyoipokea hatua ya mshambuliaji huyo kutunukiwa tuzo ya uchezaji bora ambayo hutolewa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas.

Blatter amesema hata yeye alishangazwa kumuona Luionel Messi akiitwa kwenye jukwaa kuu, kwa kigezo cha kushinda tuzi hiyo hali ambayo amesema haikumshurutisha kuamini kama kweli mshambuliaji huyo wa klabu ya Barcelona alistahili.
Amesema mshambuliaji huyo hakuonyesha kiwango kinachostahili kama ilivyo kwenye klabu yake ya Barcelona ya nchini Hispania, hivyo alikuwa tofauti na wachezaji wengine ambao alikuwa wakiwania tuzo ya mchezaji bora wa fainali za mwaka huu.

"Nilishangazwa kidogo nilipomuona Messi anakuja kupokea tuzo ya mchezaji bora," amesema Blatter, ambaye alikabidhi tuzo hiyo.
Wadau wengine wakubwa katika fani ya soka waliodhihirisha kupinga tuzo aliyopewa Lionel Messi ni aliyekuwa nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina Diego Armando Maradona pamoja na Stan Collymore kutoka nchini Uingereza.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA