MIAMI HEAT YAMSAINISHA SHABAZZ NAPIER BAADA YA LUOL DENG

Timu ya kikapu ya nchini Marekani, Miami Heat imetangaza rasmi kumsaini mchezaji Shabazz Napier kujiunga na kikosi cha Miami Heat, Napier mwenye umri wa miaka 23 anaingia Miami heat katika kuimarisha safu ya ulinzi akitokea katika ligi za vyuoni.

SHABAZZ NAPIER KATIKA PICHA

Napier anakuwa mchezaji wa pili kusainiwa Miami heat katika msimu mpya wa 2014 baada ya Luol Deng aliyekuwa akiichezea timu ya  Cleveland ambako mkali wa Miami heat LeBron James ametimukia.

Rais wa Miami heat  Pat Riley anadhibitisha uwezo wa mchezaji huyu kwa kusema kwamba  "Shabazz Napier ni MSHINDI ni mchezaji aliyekomaa mwenye uwezo wa hali ya juu sana kutoka vyuoni niliowahi kukutana nao" 

Pat Riley anaendelea kwa kusema kuwa "Si tu kwamba yeye amesaidia UConn kuchukua ubingwa na kuwa mshindi mara mbili wa NCAA lakini pia anajua hasa yale mahitaji yanayotakiwa katika ngazi ya NBA.

Napier amemaliza kwa mafanikio makubwa katika kuchezea timu za vyuo kwa muda wa miaka minne kwa kupata point 1,959 na kusaidia mara 646 katika historia ya michezo 143 aliyocheza katika misimu 9 ya ligi katika kipindi cha Summer uko Orlando na Las Vegas.

Read more here: http://www.miamiherald.com/2014/07/18/4243125/heat-bring-back-haslem.html#storylink=cpy

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA