MSANII JUX KUINGIZA RASMI BIASHARA YAKE SOKONI JULY 23


Kupitia account yake ya Instagram msanii Jux na mjasiriamali ameonyesha aina ya nguo zake mpya  yaani vest zenye picha yake ambazo anatarajia kuziingiza sokoni kwanzia tarehe 23 July,2014.

"juma_jux Vest zitapatikana duka la STARLOOK Sinza kuanzia tarehe 23 mwezi huu call or whatsaap +255652417118 @fatma8five ladies kuna size zenu pia #africanboy #25" ameandika post hii kwenye instagram kuwapa taarifa mashabiki wake kuwa mzigo huko njiani. 
 
Jux amekuwa akitwajwa mara kadhaa katika website na magazine tofauti tofauti kuwa ndio msanii anayepiga pamba kali sana hapa Bongo. Kupitia tovuti ya Bongo5 post yao ya tarehe 22 January, 2013 walimuonyesha Jux kuwa ndie msanii namba moja kwa Bling Bling hapa Tanzania, unaweza bonyeza hapa na kuona orodha ya wasanii wengine wanaonyuka pamba kali.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA