MANISPAA YA KINONDONI YAWAFUKUZA WATUMISHI TISA NA WENGINE WAWILI WAPEWA ONYO KALI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Madiwani la Manispaa yaa
Kinondoni katika Kikao chake cha tarehe 22/07/2014 siku ya Jumanne, chini ya
Mstahiki Meya Mh.Yusuph Mwenda
pamoja na mambo mengine lilijadili na kutolea maamuzi ya mashauri ya mashtaka ya
nidhamu yaliyofunguliwa kwa Watumishi 11
wa Idara mbalimbali za Manispaa waliofanya makosa mbalimbali kama Utoro kazini,
Matumizi mabaya ya madaraka na ofisi.
Kati ya Watumishi 11 waliofunguliwa Mashtaka, watumishi 6 ni wa Idara ya Afya, 2 ni wa Idara ya Elimu ya Sekondari (Walimu
wa Leseni) na 3 ni wa Idara ya
Utawala na Utumishi kada ya Maafisa
watendaji wa Mitaa ambao ni 2
na polisi msaidizi 1.
Aidha Baraza limefikia uamuzi wa
kuwafukuza kazi watumishi 9 na
kuwapa karipio watumishi 2. Kati ya watumishi 9 waliofukuzwa kazi, watumishi
4 ni wa Idara ya Afya, 3 Idara
ya Utawala na Utumishi ambao ni Maafisa watendaji wa Mitaa 2 na Polisi Msaidizi 1, na 2 kutoka idara ya Elimu ya Sekondari
ambao ni walimu wa Lesseni.
Watumishi 2 waliopewa kalipio kutoka Idara ya Afya wametakiwa kujirekebisha,
ambapo watakuwa katika uangalizi kwa muda kuona kama wamejirekebisha mienendo
yao.
Baraza la Madiwani limewataka watumishi
wote, kuzingatia sheria, taratibu, kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali ya
Serikali katika kutekeleza majukumu yao ya kutoa huduma kwa Umma sambamba na
kuheshimu maadili ya kazi zao kwa hekima na busara, ili kuweza kutoa huduma
bora kwa wakazi wa Kinondoni.
Aidha, Baraza limesisitiza kuwa
halitasita na litaendelea kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wanao fanya makosa mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
SEBASTIAN MHOWERA
AFISA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.
Comments
Post a Comment